Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, imemkabidhi tuzo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (MB) ikiwa ni njia ya kutambua jitihada na mchango wake katika kupambana na masuala ya ukatili hapa nchini.
Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Uendeshaji ya Taasisi, Dkt. Rosemarie R.N Mwaipopo kwenye Sherehe za Mahafali ya 12 ya Taasisi zilizofanyika Chuoni Tengeru, Disemba 16, 2022.
Kwa mujibu wa Dkt. Mwaipopo, Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru imeona ni vema kumkabidhi tuzo hiyo Waziri Dkt. Gwajima ili kutambua jitihada zake katika kupambana na changamoto kubwa ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Dkt. Mwaipopo amemhakikishia Waziri Gwajima kuwa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, imeamua kumuunga mkono Waziri kwa vitendo katika mapambano hayo ambapo Taasisi imeanzisha kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) kwa madhumuni ya kuhamasisha Wanafunzi kuitikia wito wa Wizara wa kuendesha kampeni ya kizalendo nchi nzima kupinga ukatili.
Mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Waziri Gwajima, alishukuru kwa na kutoa wito kwa wahitimu wa Taasisi kuhakikisha wanakuwa vinara wa kupinga ukatili katika maeneo watakayokuwa.
‘’Muitumie taaluma ya maendeleo ya jamii kutoa elimu kuhusu madhara ya ukatili’, alisisitiza Dkt. Gwajima.
More Stories
Papa Francis afariki Jumatatu ya Pasaka akiwa na miaka 88
Kanisa la Shincheonji la Yesu nchini Ufaransa lakanusha ripoti ya Le Parisie
Vyombo vya ulinzi na usalama Mbeya,Benki kuu kushirikiana kutatua changamoto za utapeli mtandaoni