January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TIC yaendelea na kampeni ya kutoa elimu masuala ya uwekezaji nchini

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TICI kimeendelea na Kampeni ya Kitaifa kwa Mikoa ya Kusini ,ambapo Mkuu wa Wilaya ya Lindi,  Shaibu Ndemanga, amepongeza jitihada zinazofanywa na kituo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya uwekezaji.

Akizungumza wakati wa kampeni hiyo wiki hii, DC Ndemanga amepongeza  jitihada na kutoa wito kwa Watanzania na wananchi wa Lindi kuchangamkia fursa hiyo.  

“Nitoa wito kwa wana Lindi na Tanzania kwa ujumla kutumia fursa hii kupata elimu, lakini pia kuchukua hatua sasa kwa kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ina lengo la kuwasaidia Watanzania si tu kwa kusajili miradi, bali pia kuona jinsi miradi hiyo inavyosaidia Watanzania, hasa katika suala zima la ajira.” Alisema.

TIC  inaendelea na kuratibu kampeni ya kitaifa yenye lengo la kuchochea uwekezaji wa ndani nchini.  Kwa sasa TIC iko katika mikoa ya Kusini ya Lindi, Ruvuma na Rukwa  na kundelea Katavi na Kigoma ikiwa ni awamu ya pili ya kampeni hiyo iliyoanza Januari 2024 kwa kupita mikoa ya kanda zote nchini.

Kampeni hiyo   imeelekeza nguvu zake katika kutoa elimu na hamasa kwaWatanzania kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini.

TIC inashirikiana na vyombo vya habari  kutoa elimu kwa umma kupitia semina zinazofanyika katika mikoa ya Tanzania. Lengo mojawapo la kampeni ni kueleza mabadilikoyaliyofanywa katika sheria ya uwekezaji ya mwaka 2022, ambayo imeweka kipaumbele kwa Watanzania katika uwekezajiwa ndani. 

Sheria hiyo inatoa fursa kwa Watanzania hususani kwa kupunguza thamani ya mtaji kwa kuwekeza kati ya dola laki 1 hadi dola elfu 50, hivyo kurahisisha uwekezaji kwa Mtanzania.

Mratibu wa kampeni hii akiwa na timu ya TIC walipokuwa mkoani Lindi walitembelea mradi Sheby Mix Investment uliosajiliwa TIC unaofanya shughuli za uchimbaji madini.



Meneja wa Uhamsishaji na Uwekezaji wa Ndani wa TIC, Felix John,  alisema kampeni hiyo inachochea mabadiliko makubwa katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini. Alisisitiza kwamba hatua hizi zitasaidia Watanzania  kuanzisha na kukuza miradi yao.