December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TFRA yawataka wakulima kutumia mbolea kwa usahihi

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzanaia(TFRA)Dkt.Stephan Ngailo amewataka wakulima nchini kulima kwa kufuata maelekezo na taratibu za matumizi ya mbolea ili kuepuka kuona mbolea wanayonunua ni bandia.

Ngailo amesema Tanzania hakuna mbolea bandia bali ni wakulima kulima na kuweka mbolea bila utaratibu nakupelekea mbolea kuondoka shambani kwa kusombwa na maji nakudhani mbolea hiyo ni bandia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo,Julai 17 ,2023 kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo Mkurugenzi huyo amesema kuwa kumekuwa na natabia ya wakulima kutumia mbolea bila kufuata taratibu za kilimo na wakishatumia na kukuta tofauti wanalalmika kuwa mbolea ni (fake) bandia.

“Wengi wanasema mbolea inaharibu udongo hii siyo kweli hata dawa usipoitumia vizuri kwa mujibu wa maelekezo itaathiri matibabu vivyo hivyo kwa mbolea inabidi itumike vizuri kwa kufuata maelekezo Tanzania hatuna mbolea (fake)bandia,

“Tanzani hatuna changamoto ya upatikanaji wa mbolea isipokuwa wakulima wamekuwa na desturi ya kuchagua aina fulani ya mbolea inapotokea imepungua au kuisha ndipo uibuka malalamiko lakini si kwamba mbolea haipo,”amesema Ngailo.

Aidha Ngailo ameeleza kuwa mpaka kufikia Juni 30,2023 upatikanaji wa mbolea ulikuwa tani 1,115,841 ambapo lengo limefikiwa na kuvuka kabla ya miaka miwili ya ilani kukamilishwa kwa asilimia 139.48.

Pia amezengumzia mpango na bajeti wa Mamlaka hiyo katika mwaka 2023/2024 ambapo amesema Serikali imetenga bajeti ya Shilingi bilioni 150 kwa ajili ya ruzuku ya Mbolea na kusema kuwa mamlaka itaendelea kuratibu na kusimamia utoaji wa ruzuku kwa wakulima, Mpango wa Maendeleo wa Kilimo wa II (ASDPII),Kuimarisha tija na faida katika kilimo kwa kuboresha upatikanaji na ufikiwaji wa pembejeo za kilkilimo.

Hata hivyo amesema kuwa kutokana na kupanda kwa bei za mbolea katika soko la dunia, Serikali ilitenga fedha kwa ajili ya kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima kwa lengo la Kupunguza gharama ya mbolea, Kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, Kuimarisha usalama wa chakula, Kuongeza upatikanaji wa malighafi za viwanda vya ndani ambapo kwasasa kuna kiwanda kimeongezeka kwa jili ya kuzalisha mbolea nchini kinachoitwa intracom.