Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeendela kuimarisha udhibiti wa mbolea feki ambazo huingia nchini bila kufuata taratibu ili kuhakikisha wakulima wanatumia mbolea bora iliyokidhi vigezo.
Ameyasema hayo leo Alhamisi Feubuari 23, 2023 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa TFRA Dkt. Stephan Ngailo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mamlaka ya utdhibiti wa mbolea Tanzania.
“Tutahakikisha tunaendelea kudhibiti wote wanaojaribu kuharibu tasnia ya mbolea na kuvuruga hizi jitihada za serikali za kuhakikisha kwamba mkulima anapata mbolea iliyo bora” amesema
Pia tumeimarisha ukaguzi kwa kuongeza ofisi za kanda ambapo sasa tuna ofisi nne ambazo ni kwa Dar es Salaam ambayo ni makao makuu, Dodoma, Mwanza na Arusha kwa kuanzisha ofisi hizo zimekuwa na manufaa makubwa kwa kutoa huduma kwa wakulima pamoja na wadau mbalimbali wa kilimo nchini.
“baada ya utashi wa kisiasa wa serikali umechochea uwekezaji wa viwanda vya uzalishaji wa mbolea hapa nchini, kabla ya mamlaka kuanza mpaka 2016 tulikuwa na viwanda vinne, lakini mpaka sasa tunaviwanda zaidi ya 16 ambavyo nivile viwanda vinavyozalisha mbolea na visaidizi vya mbolea” amesmea Mkurugenzi wa TFRA Dkt. Ngailo
Ameongezea kuwa tuna viwanda vikubwa viwili, kiwanda kimoja cha minjingo ambacho kipo manyara nacho kinaendelea na uzalishaji wake na uzalishaji unatarijiwa kuongezeka kutoka zile tani ambazo walikuwa wakizalisha chini ya asilimia 50 na sasa wanaelekea kuzalisha tani laki moja na wanalenga kuzalisha tani laki tatu kwa mwaka na kiwanda cha Ultracom nacho ni kikubwa ambacho mpaka kukamilika kwake kitakuwa kinazalisha tani milioni moja ya mbole, ambavyo zitasaidia kuongeza upatikanaji wa mbolea nchini.
Viwanda hivi vitasaidia sana kuongeza upatikanaji wa mbole nchini na kuna baadhi ya viwanda vingine vidogo vidogo vinavyozalisha mbole za majimaji kule kibaha na mbolea ya asili kule magwepande kinondoni Dar es Salaam, moshi na Morogoro, hivyo tunahamasisha watanzania na wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza kwenye tasnia ya mbolea ili kuzalisha mbolea kwa wingi na kuondoa utegemezi wa mbolea kutoka nje ya nchi.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato