Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
TAASISI ya Elimu Tanzania(TET) imewasilisha mapendekezo ya muundo wa elimu na mabadiliko ya Rasimu ya mitaala mipya kwa bodi na menejimenti ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Wasilisho hilo limefanyika Leo Oktoba 13, 2023 katika chuo cha Utalii cha VETA jijini Arusha, Lengo ni kuwapatia ufahamu Bodi na Menejimenti ya VETA kuhusu utekelezaji wa elimu ya Amali kwa Sekondari Hatua ya Chini ambapo utekelezaji wake kwa kiasi kikubwa utafanywa na kusimamiwa na VETA
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Dkt. Aneth Komba amefanya wasilisho hilo mbele ya mwenyekiti wa bodi hiyo Prof. Sifuni Mchome na wajumbe wa bodi pamoja na menejimenti ya VETA ambapo ameeleza kuwa mitaala mipya itasaidia katika kumuandaa mwanafunzi kujitegemea kwani atakuwa na uwezo mzuri kutokana na ujuzi atakaopata kupitia mabadiliko hayo ya elimu.
“Maboresho haya ya Mitaala mipya ya elimu yamefanyika kwa kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha elimu itakayomuwezesha muhitimu kuweza kujiajiri na kuajiriwa baada ya kumaliza masomo yake “amesema Dkt. Komba
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya VETA, Prof Mchome ameeleza kuwa wasilisho la Mitaala ni jambo jema kwao kuweza kupata uelewa kwa wajumbe na menejimenti nzima ya VETA na kuwa itawazesha kujipanga katika utoaji elimu kwenye eneo lao la Elimu ya Amali.
“Matarajio kwa wananchi ni makubwa kwenye maboresho ya mitaala hii hivyo ni wazi kuwa sasa kazi itaanza vyema ya kuhakikisha elimu imeboreshwa na kwamba sasa tunapaswa kujipanga vyema kama VETA alisema Prof. Mchome.
Katika hatua nyingine ,Dkt.Komba aliweza kukabidhi taarifa mbalimbali zilizofanyiwa kazi kwa VETA kupitia nakala laini (soft copy) zitakazosaidia katika utekelezaji wa rasimu ya mitaala .
Pia, katika kikao hicho, wajumbe wa bodi na Menejimenti ya VETA, wameipongeza sana WyEST na TET kwa kazi kubwa ya maboresho ya Mitaala na kuahidi kusimamia utekelezaji na kutekeleza kwa umahiri katika eneo lao la Amali.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi