December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Techno Auditors Mabingwa michuano ya NBAA, yaichapa KPMG 3-1

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online

FAINALI ya Mashindano ya mpira wa miguu ya maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania (NBAA) yamehitimishwa baada ya timu ya Techno Auditors kuibuka mabingwa kwa kuichapa timu ya KPMG bao 3-1 kwenye mchezo huo uliyochezwa uwanja wa TPDC jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya fainali hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno amesema taasisi nyingi zimekuwa zikichukulia poa michezo wakiamini inadumaza utendaji wa kazi jambo analipinga vikali.

Aidha, amesisitiza kuwa taasisi mbalimbali nchini zinatakiwa kutenga muda kwa watumishi wake kushiriki katika michezo badala ya kuwasisitiza kufanya kazi muda wote.

Hivyo, Jumla ya timu nane zilizoshiriki katika mashindano hayo huku timu ya Techno Auditors ikifanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania NBAA tangu kuanzishwa kwake.