Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kushirikiana na Kampuni ya NISSAN Tanzania wamekabidhi viatu kwa wanafunzi wanaotoka katika familia duni ambao wamekuwa wakiudhuria shule wakiwa peku Bagamoyo mkoani Pwani.
Akizungumza jana Agosti 10,2023 wakati wa zoezi hilo la makabidhiano katika shule ya Msingi Mtakuja, Meneja wa Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Alice Lukindo amesema TEA itaendelea kutafuta rasilimali kwa ajili ya kuendeleza elimu kusaidia sekta ya elimu nchini.
Amesema lengo ni kuwawezesha wanafunzi kutimiza malengo yao kwenye elimu na kwamba imekuwa ikipata wafadhili mbalimbali ambao wamekuwa wakisaidia kwenye nyanja mbalimbali za elimu.
“Msaada huu utaleta hamasa kwenye masomo yao na pia kuwaepusha na maradhi mbalimbali na tumeambiwa kwamba shule hizi zinafanya vizuri sana kitaaluma kwa hiyo tunaomba muwe makini na masomo,” Amesema
Kwa upande wake Ofisa Maendeleleo ya Jamii Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Bi.Delvin Maleko, ambaye amemuwakilisha Afisa Elimu wa Bagamoyo, amewataka wazazi na walezi kwa ujumla kuchanga kwaajili ya chakula cha watoto wao pindi wakiwa shuleni.
“Katika shule zote za Bagamoyo ni shule yenu tu ambayo watoto hawapati chakula shuleni, maji yapo limeni mboga mboga watoto wale shuleni na kwa ufaulu walionao inamaana watafanya vizuri sana kwenye mitihani ya kitaifa,” amesema
Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mtakuja iliyoko Kata ya Fukayosi Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Pascal Kitando ameishukuru TEA kwa kuhakikisha wamepata msaada wa viatu kwa wanafunzi ambao wanaishi kwenye familia za hali duni .
Pamoja na hayo amewaomba wadau mbalimbali kusaidia ujenzi wa uzio ili kukwepa uvamizi wa wanyama ambao wamekuwa wakisababisha uhalibifu wa mali za shule.Ofisa Maendeleleo ya Jamii Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Bi.Delvin Maleko akikabidhi viatu kwa baadhi ya wanafunzi wakati wa zoezi la kukabidhi viatu kwa wanafunzi ambao wanaotoka katika familia duni ambao wamekuwa wakiudhuria shule wakiwa peku Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika jana Agosti 10,2023 Bagamoyo mkoani Pwani
Ofisa Maendeleleo ya Jamii Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Delvin Maleko akikabidhi viatu kwa baadhi ya walimu wakiwakisha wanafunzi wakati wa zoezi la kukabidhi viatu kwa wanafunzi ambao wanaotoka katika familia duni ambao wamekuwa wakiudhuria shule wakiwa peku Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika jana Agosti 10,2023 Bagamoyo mkoani Pwani
Ofisa Maendeleleo ya Jamii Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Bi.Delvin Maleko akipata picha ya pamoja na walimu wakati wa zoezi la kukabidhi viatu kwa wanafunzi ambao wanaotoka katika familia duni ambao wamekuwa wakiudhuria shule wakiwa peku Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika jana Agosti 10,2023 Bagamoyo mkoani Pwani
Ofisa Maendeleleo ya Jamii Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Bi.Delvin Maleko akipata picha ya pamoja na wanafunzi wakati wa zoezi la kukabidhi viatu kwa wanafunzi ambao wanaotoka katika familia duni ambao wamekuwa wakiudhuria shule wakiwa peku Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika jana Agosti 10,2023 Bagamoyo mkoani Pwani
Ofisa Maendeleleo ya Jamii Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Bi.Delvin Maleko akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi viatu kwa wanafunzi ambao wanaotoka katika familia duni ambao wamekuwa wakiudhuria shule wakiwa peku Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika jana Agosti 10,2023 Bagamoyo mkoani Pwani
Meneja wa Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Alice Lukindo akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi viatu kwa wanafunzi ambao wanaotoka katika familia duni ambao wamekuwa wakiudhuria shule wakiwa peku Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika jana Agosti 10,2023 Bagamoyo mkoani Pwani
Afisa Elimu Msingi Bagamoyo, Bi.Wema Kajigili akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi viatu kwa wanafunzi ambao wanaotoka katika familia duni ambao wamekuwa wakiudhuria shule wakiwa peku Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika jana Agosti 10,2023 Bagamoyo mkoani Pwani
Meneja wa Mauzo na Masoko NISSAN Tanzania , Bw.Alfred Minja akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi viatu kwa wanafunzi ambao wanaotoka katika familia duni ambao wamekuwa wakiudhuria shule wakiwa peku Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika jana Agosti 10,2023 Bagamoyo mkoani Pwani
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mtakuja, Mwl.Pascal Kitando akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi viatu kwa wanafunzi ambao wanaotoka katika familia duni ambao wamekuwa wakiudhuria shule wakiwa peku Bagamoyo mkoani Pwani. Hafla hiyo imefanyika jana Agosti 10,2023 Bagamoyo mkoani Pwani.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi