December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TEA yaadhimisha wiki ya utumishi wa umma

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bahati Geuzye amekutana na watumishi wa Mamlaka hiyo kwenye Ofisi za TEA zilizopo UDOM, Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16, 2023 na kilele ni Juni 23,2023.

Katika mkutano huo watumishi wamekumbushwa kuzingatia misingi na miongozo ya Utumishi wa Umma katika utekelezaji wa majukumu yao ili kufanya kazi kwa weledi.

Geuzye amesisitiza kuwa lengo la TEA kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ni pamoja na kutoa fursa zaidi ya kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo ili kusikiliza kero, maoni, ushauri na mapendekezo katika kuchagia matokeo chanya kwenye utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa TEA amewakumbusha watumishi hao kujenga na kuimarisha umoja na ushirikiano baina yao na katika vitengo vyao ili kuimarisha mafanikio ya Mamlaka.