September 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TCU yatangaza nafasi takribani 100,000 za awamu ya pili ya udahili

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dodoma

KIATIBU Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Charles Kihampa, ametangaza kufunguliwa kwa wamu ya pili irisha la udahili kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza mwaka wa masomo 2024/2025 kuanzia jana ambapo nafasi 1,000 zipo wazi kwenye vyuo 86 nchini vyenye sifa ya kupokea wanafunzi wa shahada ya kwanza.

Prof. Kihampa ametangaza kufunguliwa kwa awamu ya pili ya dirisha hilo wakati akizungiza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana.

Alisema awamu ya pili ni kwa ajili ya wanafunzi mbao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa katika awamu ya kwanza kutokana na sababu mbalimbali.

Prof. Kihampa waliwata wanafunzi hao kutumia nafasi hiyo vizuri kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda, huku akielekeza vyuo vya elimu ya juu kutangaza programu ambazo bado zina nafasi.

Aliwataka waombaji kuzingatia utaratibu wa udahili wa awamu ya pili kama ilivyooneshwa kwenye kalenda ya udahili iliyoko katika tovuti ya TCU. “

“Tunawakumbusha waombaji udahili wa shahada ya kwanza kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika,” alisema.

Aidha, alisema kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa.

Prof. Kihampa alisema kwa waombaji ambao wamepata chuo zaidi ya kimoja wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimoja na mwisho wa kufanya hivyo ni Septemba 21, 2024.

“Nitoe wito kwa waombaji ambao wamepata vyuo zaidi ya kimoja, kuwa watapokea ujumbe mfupi wa kupitia simu walizotumia wakati anaomba au watatumiwa code (namba maalumu ya siri) na pia itatumwa kwenye email (anuani ya barua pepe) ambayo wanatakiwa kuitumia kujithibitisha.

Sasa amepata chuo X na amepata chuo Y achakuge anakwenda chuo gani,” alisema. Kwa mujibu wa Prof. Kihampa alisema wale ambao hawatakuwa wamepata ujumbe mfupi, lakini wamepata udahili kwenye vyuo zaidi ya kimoja wanapaswa kuingia kwenye mfumo wa udahili wa vyuo vilivyomdahili na kuomba kutumia ujumbe mfupi wenye namba maalumu ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.

Kwa mujibu wa TCU waliochaguliwa kwenye udahili wa awamu ya kwanza udahili wao umekamilika na majina ya waliodahiliwa katika awamu hiyo yanatangazwa na vyuo husika.

Katika awamu hiyo jumla ya waombaji 124,286 walituma maombi ya kujiunga katika vyuo 86 vilivyoidhinishwa kudahili wanafunzi katika shahada ya kwanza.

Kati ya waliotuma maombi ni 98,890 sawa na asilimia 79.6 ndiyo wamepata udahili kwenye vyuo walivyoomba ikiwa na maana nafasi takribani 100,000 bado ziko wazi, kwani wanafunzi 198,986 ndiyo wanaohitajika.

Idadi ya nafasi zilizopo katika mwaka wa masomo unaotarajiwa kuanza mwaka huu ni ongezeko la asilimia 6.8 ikilinganishwa na nafasi 186,289 mwaka uliopita zilizokuwapo kwa ajili ya shahada ya kwanza.

“Idadi ya waombaji wa udahili watakaodahiliwa inatarajia kuongezeka katika awamu ya pili ya udahili,” alisema Profesa Kihampa.

Mbali na kuongezeka kwa nafasi za masomo, alisema programu zinazotolewa na vyuo zimeongezeka hadi kufikia 856 ikilinganishwa na programu 809 mwaka 2023/2024, ikiwa ni ongezeko la programu 47 za masomo.