December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TCCIA yataka wadau washiriki mkutano wa Halal

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

CHEMBA ya  Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), kimetoa wito kwa wafanyabiashara kote nchini kushiriki mkutano utakaotoa elimu ya bure kuhusu namna ya kupata cheti cha Halal kwenye bidhaa zao.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA, Oscar Kisanga, wakati akizungumzia mkutano huo utakaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alisema TCCIA inawanachama nchi nzima na imekuwa ikishirikiana na serikali bega kwa bega kuhakikisha mazingira ya biashara yanaboreshwa na wafanyabiashara wanafurajia kazi zao.

Alisema chemba hiyo inawanachama nchi nzima walioko kwenye makundi tofauti tofauti na kwamba miongoni mwa wanachama wa TCCIA ni MICO International Halal ambaye amekuwa akilipa ada zake bila tatizo.

“Moja ya  huduma zinazotolewa na TCCIA ni kutoa vyeti kwa wafanyabiashara nchini kuuza bidhaa zao nje ya nchi yaani Certificate of Origin  na wenzetu MICO  Halal ambao ni wanachama wetu nao wancheti wanachotoa kwenye bidhaa mbalimbali,” alisema

“Awali walianza na kutoa Halal kwa wafanyabiashara wa nyama lakini wanatoa cheti cha Halal kwa bidhaa mbalimbali na walezi wao ni Baraza Kuu la Waislamu BAKWATA na kesho MICO Halal kesho Jumatano watakuwa na mkutano unaoitwa  Tanzania Halal Business Summit nan i kongamano la bure watu wote wanaruhusiwa kuhudhuria,” alisema

Alisema lengo la kongamano hilo ni kuwapa elimu wadau kuhusu utaratibu wa kupata cheti cha Halal ili waweze kusafirisha bidhaa mbalimbali kwenye mataifa yote duniani ambayo yamekuwa yakitoa kipaumbele kwenye bidhaa zenye cheti cha Halal.

“Nawakaribisha watu wote kwenye mkutano huo na sisi TCCIA tunawaunga mkono kwasababu mlezi wao mkubwa ni BAKWATA Tanzania na natoa shukrani kwa serikali ya Tanzania kwa kuendelea kufungua milango na fursa mbalimbali kwa wafanyabaishara,” alisema