Benki ya Biashara Tanzania (TCB) leo imesaini mkataba wa makubaliano (MOU) naWakala wa serikali wa uwezeshaji wananchi kiuchumi zanzibar ( ZEEA) Makubaliano haya ya kimkakati yanalenga kuanzisha mpango maalum wa mikopo utakaonufaisha makundi maalum wakiwemo wanawake na vijana wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi visiwani Zanzibar.
Mpango huu unakusudia kuchochea ukuaji wa biashara, ongezeko la ajira, na maendeleo ya kiuchumi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Akishuhudia kusainiwa kwa hati hizo jijini Dar es salaam Katibu mkuu ofisi ya Raisi kazi uchumi na Uwekezaji zanzibar Mariam amesema tayari shilingi bilioni 2 zimeshakusanywa na halmashauri visiwani humo ili kuanza uwezeshaji akiitaka benki ya TCB kuhakikisha inafanya tathmini ya mikopo wanayotoa kwa makundi hayo ili ziweze kurejeshwa kwa wakati na wengine waweze kukopa .
Ameeleza kuwa mpango huu wa mikopo umekusudiwa kutia chachu juhudi za kijasiriamali,kuwapa wajasiriamali uthubutu wa kuanzisha na kupanua biashara zao. Malengo ya uwezeshaji huu ni kuwa chanzo cha mabadiliko mengine kama kuimarisha
uchumi wa ndani, kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupambana na ukosefu wa ajira na kuleta maendeleo na kuwa Kupata fursa ya mikopo ni muhimu kwa maendeleo na ukuaji wa biashara
ndogondogo na za kati
Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa TCB ADAM MIHAYO amesema Mkataba huu wa makubaliano unathibitisha dhamira ya Benki ya TCB kuwezesha uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla na kwamba Mkataba huu wa makubaliano unathibitisha dhamira ya Benki ya TCB kuwezesha
uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla.
Amesema mkataba huo utawezesha kutoa mikopo nafuu kwa makundikiasi cha shilingi milioni 30 kwa kikundi, huku wakipewa muda miezi 24 sawa na
miaka miwili Kwa kutoa mikopo nafuu
kwa makundi hayo, TCB na ZEEA watawasaidia wajasiriamali kupanua biashara zao, kutengeneza fursa mpya za ajira, na hivyo kupunguza uhaba wa ajira.
Mpango huu pia utazisaidia biashara kujiendesha, kukabiliana na mfumuko wa bei, pamoja na kuwekeza katika vitendea kazi, na kuzipa ustahimilivu,Tuna furaha kushirikiana na ZEEA kuwainua wajasiriamali wanawake, vijana na makundi mengine maalum yaliyomo visiwani Zanzibar,” alisema Adam Mihayo,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB.
Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa ZEEA Juma Burhan Mohamed amesema wanalenga kuipatia benki ya TCb kiasi cha shilingi bilioni 1.8 ili waanze utoaji wa mikopo hiyo na kwamba Mpango huu unaendana na lengo la kuwezesha maendeleo ya kiuchumi kwa kujenga uchumi jumuishi Kwa
kuyawezesha makundi maalum, wanaziinua biashara binafsi, pamoja na kuimarisha mfumo mzima wa uchumi na kutengeneza mazingira imara ya
kiuchumi.” alisema
Mbali na kuchangia maendeleo ya kiuchumi, makubaliano haya pia yanakusudia kuimarisha uchumi wa buluu visiwani Zanzibar. Kupitia mikopo hii itakayoinua biashara ndani katika sekta hii, TCB na ZEEA wanapigia chapuo eneo hili nyeti la
shughuli za kiuchumi lenye uwezo wa kuchangia maendeleo kwa kiasi kikubwa.
Mchango wa Benki ya TCB katika kuunga mkono jitihada za Serikali katik na kupokea maombi ya mkopo yanayofikia wastani wa Mpango huu wa mikopo umekusudiwa kutia chachu juhudi za kijasiriamali, kuwapa wajasiriamali uthubutu wa kuanzisha na kupanua biashara zao Malengo ya uwezeshaji huu ni kuwa chanzo cha mabadiliko mengine kama kuimarisha biashara na uchumi
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa