Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam
BENKI ya Taifa ya Biashara (TCB) imeanzisha kampeni ya kopa maji yenye lengo la kumrahisishia mwananchi kupata huduma za maji safi na usafi wa mazingira kiurahisi katika jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo,Mkurugenzi wa Mikopo Benki hiyo, Henry Bwogi amesema huduma hiyo ya Mikopo imewalenga watu binafsi na Taasisi mbalimbali.
Amesema kampeni hiyo inatarajia kuanza kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia septemba mpaka Desemba mwaka huu katika mikoa mbalimbali .
Bwogi amesema utoaji wa mkopo huo utaenda sambamba na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu namba 6 ya upatikanaji wa Maji safi na usafi kwa wote.
“TCB imekuwa mstari wa mbele katika kuja na huduma za kibunifu na zenye kuongeza tija katika kuboresha maisha ya mtanzania TCB ilipata ufadhili kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya Water Org ya Marekani Ili kuiwezesha Benki kutengeneza na kuanza kutoa Mikopo kwa ajili ya kuwasaidia watanzania katika upatikanaji wa maji” amesema Bwogi
Akiyata makundi ambayo yanufaika na mkopo huo ni pamoja Mikopo ya mtu mmoja mmoja ambao utamwezesha kukopa kwa ajili ya kwenda kuunganisha Maji kwenye majumba yao, mashirika na taasisi ambazo zinakopa kwa ajili ya shughuli mbalimbali zinazohusiana na upatikanaji wa maji kama vile wakandarasi wenye kandarasi kwenye miradi ya Maji.
Bwogi amesema kundi jingine ni kwa ajili ya wafanyabiashara wanahousika na uuzaji wa vifaa mbalimbali vinavyotumika katika kuunganishia wananchi maji kama wauzaji mabomba na vifaa vingineno.
Vilevile amesema wachimbaji visima nawasafirishaji wa Maji taka nao ni miongoni mwa wananufaika wa Mikopo hiyo.
“Mikopo hii itakuwa na riba tofauti na nafuu kulingana na aina ya mkopo ambao mteja anachukua unaagukia katika kundi gani …ili kuweza kufaidi mikopo hiyo mteja anatakiwa kwanza kuwa na akaunti ya TCB “amesema Bwogi
Aidha amesema kupitia kampeni hiyo TCB imejipanga kuwafikia watanzania elfu 61000 na kutoa Mikopo takribani elfu 6000 yenye thamani ya shilingi billioni 8.3 kufika mwisho wa mwaka 2025.
Bwogi amesema Kampeni hiyo itafanyika katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya pamoja na Dodoma na baadae itaendelea katika mikoa yote ya Tanzania kwa ajili ya kuamasisha umma kuhusu kopa Maji na manufaa yake
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja