December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tawi la chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) mbeya kuzinduliwa Septemba 24 mwaka huu.

Na David John, Timesmajira Online, Mbeya

MKUU wa Chuo cha Elimu ya Biashara Tanzania (CBE) Profesa Emanuel A Mjema amesema chuo hicho ni kikongwe hapa nchini kwani kimeazishwa mwaka 1965 na kina matawi mkubwa manne ambapo tawi kubwa kabisa lipo jijini Dar es Salaam Dodoma,Mwanza,na tawi la mbeya hivyo tawi la mbeya sasa hivi wameshahamia katika maeneo ya chuo na ujenzi umekalika kwa asilimia 98 na wamebakisha sehemu chache hususani katika mazingira ya nje.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chuo hicho kilichopo jijini Mbeya katika maeneo ya iganzo Profesa ,Mjema amesema kuwa wanatarajia kukamilisha ujenzi huo Agosti 30 mwaka huu na uzinduzi rasim utafanyka tarehe 24 septemba na kilkichobaki ni kujenga mabweni ya wasichana.

Amesema kuwa katika kukamilisha kwa ujenzi huyo kuna wadau wengi wamejitokeza katika kuchangia wakiwamo NMB,wamechanga mabati mengi sana TBS lakini bila kuwasaha u wafanyakazi wa chuo hicho pamoja na wadau wengine wengi hivyo wanawashukuru sana kwa kujitoa kwao kwa ajili ukamilishaji wa chuo hicho.

“Tunamshukuru sana mkuu wa mkoa wa Mbeya Comred Juma Homera kwani ameweza kuchangia shilingi milioni tano hivyo tuna mshukuru lakini Angelina ndelula naye amehaidi mifuko mingi sana na vyombo vyua habari kwa kuweza kutangaza .”amesema

Pia amewaomba wadau kuendelea kuchangia harambee hiyo kwa ajili ya kujenga mabweni hayo ya watoto wa kike kwani wakipata mabweni wataweza kujisomea na kuelewa kuliko wakikaa mtaani ambapo ni rahisi kupata madhara mengi na ndio maana wametaka mabweni hayo.

Akizungumzia gharama za mradi huo Profesa Mjema amesema kuwa hadi hapo walipofikia wametumia shilingi bilioni moja na zaidi na bado wanahitaji shilingi bilioni moja nyingine kwajili ya kujenga mabweni.

Amefafanua kuwa kwa sasa bado hawajaaza ujenzi wa mabweni na ndio maana wanahamasisha wananchi pomoja na taasisi zingine kuendelea kuchangia ili kumfanya mtoto wakike kuweza kuepukana na vishawishi kwani watoto hao wanakutana na changamoto nyingi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa tawi la chuo cha elimu ya biashara Jijini Mbeya Jeremiah w Tumain amewataka wanafunzi waliomba kujiunga na chuo hicho wafike chuoni hapo kwa ajili kupata utaratibu wa kujiunga katika mwaka wa masomo unaoza mwezi wa tisa mwaka huu.

Ameongeza kuwa chuo hicho kipo hatua za mwisho ya kukamilisha ujenzi wake hivyo wanafunzi wanaohitaji kujiunga na masomo udahili unaendelea hivyo wanakaribishwa sana kujiunga na chuo hicho.