Na Mwandishi wetu,TimesMajira,Online
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Jenerali (rtd) Davis Mwamunyage amesema tatizo la maji kwa wakazi wa Kigamboni na Mkuranga litamalizika mapema mwakani, 2021.
Mwamunyange ambaye pia ni Mkuu wa Majeshi mstaafu, amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA katika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam na Mkuranga, Mkoani Pwani.
Amesema, anatambua hitaji la maji kwa wananchi wa maeneo hayo hivyo na umuhimu wake kwa maendeleo hivyoamewahakikishia wananchi wa maeneo hayo kuwa, Mamlaka anayoisimamia inakwenda kumaliza changamoto hiyo kwa haraka ili adha huduma ya maji safi na salama ibaki kuwa historia.
Mwamunyange amesema, kwa sasa ujenzi wa miradi hiyo inaendelea katika hatua nzuri, wakandarasi wanaendelea kwa kasi ambapo hadi kufikia Aprili 2021 hitajio la maji kwa wananchi hao litakuwa limepatiwa ufumbuzi.
“Mradi huu wa Kimbiji ni moja ya miradi mkubwa na ya kimakakati mradi utamaliza tatizo la maji kwa eneo la Kigamboni na baadhi ya maeneo ya Temeke,”amesema na kuongeza
“Kuhusu mradi mkubwa wa maji wa Mkuranga, maji yatakayozalishwa yatatosheleza ongezeko la idadi ya watu na mahitaji ya viwanda kwa muda mrefu ujao,”amesema
DAWASA inatekeleza mradi wa Maji katika mji wa Mkuranga unaogharimu kiasi cha Sh. 5.5 bilioni na utahudumia wakazi takribani 25,000 huku katika Manispaa ya Kigamboni unatekeleza kwa gharama ya Sh. 8.7 bilioni unaolenga kuhudumia wakazi 450,000.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa