November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TAS wapaza sauti tukio la kutekwa mwenye Ualbino

Mwenyekiti wa TAS Taifa Godson Mollel aliyevalia miwani akielezea kuguswa na kikerwa kwa tukio la kuvamiwa na kutekwa mtoto mwenye ualbino Asimwe Novat na watu wasiojulikana Muleba Mkoani kagera

CHAMA cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) wanalani vikali tukio la kuvamiwa,kuchukuliwa kikatili na kupelekwa kusikojulikana kwa Asimwe Novat ambaye ni mtoto mwenye ualbino mwenye umri wa miaka 2 na nusu katika eneo la Mbale wilaya ya Muleba Mkoani Kagera.

Akizungumza jijini Dar es salaam mwenyekiti wa TAS Taifa Godson Mollel amesema tukio Hilo la kikatili lilitokea mei 30 mwaka huu ambapo mama wa mtoto alivamiwa na wahalifu nyumbani kwake majira ya saa 2 za usiku.

“Walibisha hodi huku wakijitambulisha kuwa wanaomba chumvi wamegongwa na nyoka ndipo mama wa Asimwe alifungua milango ndipo wahalifu waliingia ndani na kumkaba koromeo huyo kisha walimchukua Asimwe na kutokomea naye pamoja na simu ya mama yake,”amesema Mollel

Aidha mwenyekiti huyo amesema kuwa kitendo hiki ni cha kikatili dhidi ya mtoto asiye na hatia sio tu cha kuchukiza bali kinaonyesha kiwango cha ushirikina uliokithiri katika jamii yetu na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo mwenyekiti huyo amesema chama cha watu wenye ualbino Tanzania wanasimama na Asimwe Novato pamoja na famiia yake katika kipindi hiki kigumu ambacho hawajui yupo katika mazingira gani kutokana na vitendo hivyo vya kinyama.

Amesema wanapongeza mwitiko wa haraka wa serikali na wadau wa watu wenye ualbino kwa kuonyesha kusikitishwa na kuchukiza na kitendo hiki cha kuchukuliwa kwa nguvu hatimae kupelekwa kusiko julikana uchaguzi wa kina wa kumtafuta Binti aliyechukuliwa unaendelea.

Kutokana na hali hivyo wameomba serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana wadau na watu wenye ualbino Tanzania na wanakijiji wa Mbale kuhakikisha mtoto huyo anapatikana.

Pia wameomba serikali ifanye uchaguzi Ili kubaini waganga wanaofanya kitendo cha kupiga ramli chonganishi zinazochochea ongezeko la matukio ya kikatili dhidi ya watu wenye ualbino vilevile ichunguze kwa kina dhidi ya tukio Hilo na kuhakikisha wahusika wanafikishwa mahakamani.