January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanzania, Zambia kuondoa vikwazo vya biashara

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema wameazimia kuweka mazingira yatakayofanya biashara kati ya Tanzania na Zambia zisiwe na vikwazo.

Wakizungumza katika Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Zambia lililofanyika jana jioni marais hao walisema eneo moja la muhimu ni kuhakikisha magari hayakai kwenye mipaka kwa muda mrefu pasi na sababu.

Marais hao wanakutana kwenye mkutano wa ana kwa ana leo asubuhi na waliwaambia Wafanyabiashara hao kwamba mazungumzo yao yatajikita kwenye kuweka taratibu za kuondoa changamoto hizo.