January 27, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanzania yatajwa namba nane Afrika kuzalisha mitaji ya kibunifu ya TEHAMA

Na Zena Mohamed, Timesmajiraonline,Dodoma.

TUME ya TEHAMA imesema Tanzania ni nchi ya nane Afrika na nchi ya Pili Afrika Mashariki katika takwimu za idadi ya nchi ambazo zinazalisha mitaji ya kibunifu ya TEHAMA.

Hayo yamesemwa jiji hapa leo,Agosti 25,2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo,Dkt.Nkundwe Mwasaga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa shughuli na mafanikio ya tume hiyo ambapo amesema Tanzania inafanya vizuri katika kuzalisha mitaji ya kibunifu Afrika.

Dkt.Nkundwe amesema kuwa tafiti zilizofanywa na taasisi ya umoja wa mataifa inaitwa ITU kuangalia jinsi ya shughuli za kidigitali ambazo zipo salama zaidi au wanavyopima kuhusiana na mambo ya usalama mtandaoni ( cirber security )Tanzania iliibuka namba mbili huku ya kwanza ikiwa Morishazi.

Amefafanua kuwa sababu hizo za kiusalama wa mtandao ndiyo chanzo cha Tanzania kuwa nafasi ya nane Afrika katika kuzalisha mitaji ya kibunifu kwani Kampuni nyingi zimekuwa zikivutiwa kuwekeza Tanzania.

” Kwasabab Kampuni hizi zina tabia moja ,hazipendi kwenda kuwekeza kwenye sehemu ambayo haina usalama,sisi Tanzania tupo vizuri ndiyo maana zinakuja kuwekeza kwetu,”amesema Mkurugenzi huyo.

Aidha Dkt.Nkundwe amesema kuwa TEHAMA imesaidia masuala mbalimbali hapa nchini ikiwemo huduma za fedha kupitia benki ambapo mwananchi anaweza kufanya shughuli za kibenki bila kufika benki na hadi sasa tume imeshasajili wataalam wa TEHAMA 1,600 wanaohudumia nchi nzima.

Akizungumzia vipaumbe vya Tume hiyo kwa mwaka 2023/24 Dkt.Nkundwe amesema kuwa tume hiyo itaendelea na ukamilishwaji wa vituo vya ubunifu TEHAMA (Soft centers) katika Kanda 5 pamoja na kuanzisha kituo kimoja Zanzibar,kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya TEHAMA (ICT Refurbishment and Assembly centre),kuwezesha uanzishaji wa vituo vya majaribio vya ubunifu TEHAMA (District ICT Startups Innovation hubs) katika Wilaya 10.

“Kufanya tafiti za maendeleo ya TEHAMA nchini na kufanya tathmini ya kitaifa ya hatua za utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya TEHAMA pamoja na Kuratibu na kuandaa matukio ya kuvutia uwekezaji na kutangaza masoko ya bidhaa za TEHAMA ndani na nje ya nchi,Kushirikiana na washirika wa maendeleo na kampuni za kimataifa katika kuendeleza bunifu za TEHAMA ikiwemo kuwezesha utengenezaji wa bidhaa za TEHAMA hapa nchini,”amesema.