December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanzania yapokea magari 10 yakubebea wagonjwa

Na Mwandishi wetu, timesmajira

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo Octoba 4,2023 amepokea magari 10 ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya Shilingi Bil. 1.1 kutoka Serikali ya India.

Waziri Ummy ameishukuru Serikali ya India kupitia kwa Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Pradhan kwa msaada huo ambao unaendelea kuonesha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

“Serikali ya India imekua na ushirikiano Mkubwa na Serikali ya Tanzania ikiwemo katika Sekta ya Afya, hivyo nitumie fursa hii kuwashuku sana kwa msaada wa magari haya ambayo hata kwenda kusaidia kurahisisha huduma kwa Watanzania”.Amesema Waziri Ummy