Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema Tanzania inakaribisha wawekezaji wote wa madini mkakati na kuweka msisitizo kwamba uongezaji thamani wa madin hayo mkakati lazima ufanyike Tanzania.
Mavunde ameyasema hayo leo Bali,Indonesia wakati wa majadiliano juu ya manufaa ya Madini Mkakati katika kukuza uchumi wa nchi wazalishaji ikiwa ni sehemu ya mkutano wa jukwaa la INDONESIA AFRIKA.
Waziri Mavunde ameonesha dhamira njema na mazingira mazuri yaliyowekwa na serikali chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuvutia uwekezaji nchini na hivyo kuwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika uchimbaji wa madini mkakati ambayo yana mahitaji makubwa duniani na Tanzania imebarikiwa nayo.
Waziri Mavunde amesisitiza kuwa kwasasa ni sharti la lazima kwamba madini mkakati hayo yaongezwe thamani nchini ili kuvutia viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo betri ya magari ya umeme.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria