WAZIRI wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), ameongoza Ujumbe wa Tanzania ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Mkutano huo umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania- TRA, Bw. Mcha Hassan Mcha, Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja