Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade ) kwa kushirikiana na Shirika la Posta nchini wametoa mafunzo kwa wajasiriamali wanawake 50 Â kutoka kutoka vikundi mbali mbali katika Wilaya ya Temeke wenye lengo la kuwajengea uwezo juu ya kutambua fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi.
Mafunzo hayo yaliyotolewa leo Jijini Dar es Salaam katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) ni muendelezo ya mafunzo ya siku ya Wanawake yaliyofanyika Visiwani Zanzibar tarehe 8 Machi siku ya kilele cha siku ya Wanawake duniani.
Meneja wa Uendelezaji wa Biashara ndogo na za kati kutoka TanTrade Crispine Luanda alifungua mafunzo hayo kwa kueleza nafasi ya Tantrade katika kuwaendeleza wajasiriamali wadogo na wa kati katika kutumia fursa zilizopo ndani na nje ya nchi.
Naye Afisa Biashara (Uendelezaji biashara ndogo na za Kati) Deo Shayo alitumia fursa hiyo kuwaonesha fursa na  mbinu za kukuza masoko ambayo ni Pamoja na kuongeza thamani ya bidhaa zao na pia kuhudhuria katika maonesho mbali mbali ya biashara ili kutanua masoko na kupata uzoefu wa kibiashara, kujisajili na kuuza bidhaa kupitia maduka mitandao amb ayo kwa Tanzania inasimamiwa na shirika la posta Tanzania.
Kwa upande wake Afisa Masoko kutoka shirika la posta Tanzania Rose Mafuru  alitumia nafasi hiyo kuonesha namna ambavyo wajasiriamali hao wanaweza kunufaika na huduma zinazotolewa na shirika la Posta chini ambayo ni Pamoja na duka Mtandao (E-Shop) ambapo mfanyabiashara anaweza kuuza bidhaa yake kokote duniani jambo ambalo litawaongezea mapato na kukuza biashara zao.
Naye Afisa uendelezaji wa biashara ndogo na za kati kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Deo Shayo, afisa kutoka Tantrade, ameonyesha mbinu za kukuza masoko ambayo ni Pamoja na, kuhudhuria katika maonesho mbali mbali ya biashara ili kutanua masoko na kupata uzoefu wa kibiashara, kuhudhuria mikutano ya kibiashara Pamoja na kujisajiri na  kuuza bidhaa kupitia shirika la posta Tanzania.
Luanda aliwasisitiza wajasiliamali hao kuondoa uwoga  katika kufanya biashara kwa kushirikiana pia amewakaribisha wajasiriamali hao katika Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) kutatua changamoto zozote za kibiashara endapo watakutana nazo na kuzipatia utatuzi. ‘’ ukitaka kufika haraka nenda peke yako lakini ukitaka kufika mbali zaidi  nenda na wenzako’’ aliongeza Luanda.
Jackline Richard ambaye ni mjasiriamali katika soko la stereo alisema, alitumia fursa hiyo kuwashukuru waandaaji kwa kuwaandalia mafunzo hayo ambayo yamewajengea uwezo mkuwa wa kujiamini , kujua fursa zilizopo Pamoja na kugundua mbinu mpya za kibiashara
‘’tunawashukuru sana kwa kutuandalia mafunzo haya, tumejifunza mambo mengi sana kuhusu biashara na ujasiriamali kupitia mafunzo haya ambayo yamesababisha tupige hatua moja mbele katika kukuza biashara zwetu’’ aliongeza Rose.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ina jukumu la kusimamia na kuendeleza biashara za ndani na nje ya nchi imekuwa ikiwafikia wajasiriamali na wafanyabiashara katika makundi tofauti ili kuwaonesha fursa zilizopo na pia njia za kufanya biashara za kiushindani.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi