January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TanTrade yapokea ugeni wa wafanyabiashara kutoka Uturuki

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Maafisa Fatuma Mapunda na Eliabu Rwabiyago kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) wapokea msafara wa wafanyabiashara kutoka Nchini Uturuki ikiwa na uwakilishi wa makampuni zaidi 31.

Msafara huo ni mahususi kwa ajili ya kuangalia fursa za kibiashara Nchini Tanzania Katika sekta mbalimbali kama Matunda na mbogamboga, Ujenzi, Ngozi, Mavazi, Bidhaa za misitu, vipuri vya magari, zana za kilimo.