December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANTRADE yakusanya asilimia 76 ya mapato


Na Jackline Martin, TimesMajira Online

KWA kipindi cha miaka mitano, Tantrade
ilipanga kukusanya ya sh. 52,562,298,340 na imefanikiwa kukusanya sh. 40,00,4650,548 sawa na asilimia 76 kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ruzuku kutoka Serikali kuu kwaajili ya mishahara na miradi ya maendeleo
na vyanzo vya mapato ya ndani.


Hiyo ni pamoja na ada inayotoza kwenye
uratibu na usimamizi wa maonesho, upangaji wakati usio wa maonesho pamoja na ushiriki wa viingilio.


Hayo aliyasema Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania (TANTRADE), Latifa Khamis, wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo jana.


Alisema Tantrade inaendelea kutekelezeka
majukumu yake kwa weledi ili kufikia dhamira ya Serikali ya awamu ya sita ya kuwa kitovu cha biashara kwa kuendeleza, kukuza na kutangaza bidhaa na huduma ndani na nje ya nchi .


Alisema hadi sasa Tantrade imefanikiwa
kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara 6,979 kupitia programu 26 ili kuimarisha uwezo wa kujiendesha kiushindani.


Pia alisema Tantrade imekamilisha maombi ya ufadhili ya kuendeleza rajamu ya Taifa ya viungo kwa kushirikiana na kituo Cha biashara Cha Kimataifa (TIC) pamoja na Sekta ya viungo.


“Hadi Agosti 2023 Tantrade imekamilisha
rajamu ya iliki, tangawizi, mdalasini, pilipili
manga na karafuu, vilevile Mamlaka inaendelea na taratibu za kukamilika rajamu za bidhaa nyingine ikiwemo, asali, korosho, kahawa na chai”


Kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa
majukumu ya Mamlaka hiyo, Latifa alisema wamefanikiwa kuratibu matukio mbalimbali ikiwemo programu za utafiti, makongamano na misafara ya kibiashara, maonesho na mikutano ya kuunganisha wazalishaji na wanunuzi ambapo ndani yake yamezaa matunda ya kuongeza uchumi nchini


“Kampuni ya Akros Cashew ya Tanzania
imeuza Tani 37 za korosho zenye thamani ya Dola za kimarekani 202, 700 zimeuzwa kupitia maonesho yaliyofanyika nchini Afrika Kusini”


“Kampuni za Tanzania zilifanikiwa kufanya mauzo ya papo kwa papo yenye thamani ya Dola za kimarekani 100,000 kwa bidhaa mbalimbali za kilimo na pembejeo kupitia msafara wa Malawi, lakini pia kampuni ziliweza kupata miadi ya mauzo yenye jumla ya thamani
ya Dola za kimarekani 20.3 kupitia msafara wa Malawi”