January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANESCO washeherekea siku ya wanawake duniani na watoto wa kituo cha UMRA

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

KATIKA kuadhimisha siku ya wanawake duniani WANAWAKE kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wamesheherekea siku hiyo kwa kujumuika na watoto wa kituo cha Kulelea watoto cha UMRA kilichopo Magomeni Mikumi Jijini Dar es Salaam kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kama njia ya kuonesha upendo.

Pia wanawake hao wametoa wito kwa wadau mbalimbali ikiwemo mashirika binafsi, Taasisi mbalimbali kujitoa kwaajili ya watoto wenye mahitaji na kutowaachia watu wachache kuwalea watoto hao.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi misaada ya Vitu mbalimbali katika kituo hicho, Jijini Dar es salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake Tanesco Makao Makuu, Prisca Maziwa amesema kuwa msaada huo ni nguvu za pamoja za Shirika hilo.

Amesema ikiwa ni kilele cha siku ya kimataifa ya wanawake wameona ni vema kujitokeza na kuungana na watoto hao katika kusheherekea siku hiyo kwa kuwapa upendo na faraja sambamba na kuwapatia vitu mbalimbali.

“Leo ni siku ya wanawake duniani tumeona ni vema kuwa karibu na jamii kwa kuwatembea watoto na kuungana nao katika kuadhimisha siku ya wanawake kwa kuwaletea mahitaji mbalimbali”amesema Prisca.

Akitaja baadhi ya vitu walivyotoa katika kituo hicho Mchele, sukari, Mafuta, Maharage, Chumvi, Mtungi wa gesi, vinywaji, Sabuni na vitu ambavyo vinatumika kijamii.

Aidha aliwapongeza wafanyakazi wa Tanesco makao makuu pamoja na wanawake wa vituo vya kufua umeme na kampuni tanzu za tanesco kwa kufanikisha kupata vitu mbalimbali kwaajili ya watoto yatima.

“Tumekuwa tukitoa misaada kadri mungu anavyokujalia katika kituo hichi au vituo vingine kusaidia katika mahitaji muhimu ya binadamu na kutoa faraja na Upendo kwa watoto hawa.” amesema Prisca.

Kwa upande wake Mwasisi wa UMRA Orphanage Centre, Rahma Kishumba amewashukuru wafanyakazi wa Tanesco kwa kutoa misaada mbalimbali kwa kuweza kuwasaidia ulezi wa watoto.

“Sinabudi ya kusema wakinamama wa Tanesco Mungu awajalie na awalipe na kila rakheri na shukrani kwa Mkurugenzi wa Tanesco.” amesema Kishumba

Abrakim Mohamed ni mmoja wa watoto wanaoishi katika kituo hicho cha UMRA amesema Wafanyakazi hao waawake wameonesha moyo wa upendo na kuwatakia mema katika majukumu yao ya kazi.

Mwenyekiti wa kamati ya wanawake Tanesco Makao Makuu Prisca Maziwa akimkabidhi mtugi wa gesi Muasisi wa kituo cua UMRA Orphanage Center Rahma kishumba
Wanawake kutoka Shirika la umeme Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaoishi katika kituo Cha kulea watoto Cha UMRA kilichopo Magomeni