December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANESCO Ruvuma yatahadharisha wananchi kuhusiana na matapeli

Na Cresensia Kapinga, TimesmajiraOnlin, Ruvuma

AFISA Uhusiano wa Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Ruvuma, Allan Njiro, amewataka wananchi wa vitongoji vya Matemanga na Mkurusi kuwa makini matapeli wanaopita kwenye nyumba zao kwa lengo la kuwaingizia umeme na kuwatoa fdha nyingi na taratibu za shirika.

Vitongoji hivyo vya Matemanga na Mkurusi vioo katika Kata ya Kigonsera Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Vijijini mkoani Ruvuma.

Ametoa tahadhari hiyo leo kwenye ziara yake ya kutoa elimu, kusikiliza kero na kutatua changamoto mbalimbali zinazohusu umeme kwa wananchi.

Amewataka wananchi hao kuchukuwa tahadhari dhidi ya matapeli ambao wanapita kwenye nyumba zao na kuwatajia gharama za kuwaingizia umeme, wakati Serikali inagharamia na wao wanatakiwa kulipia kiasi cha sh. 27,000 tu na si vinginevyo.

“Niwaombe wananchi kuwa makini na mtu atakaye kuja akitaka pesa kiasi cha sh. 100,000 au 50,000 ili akuingizie umeme, huyo ni mwizi hivyo unatakiwa kutoa taarifa kwa mtendaji wa Serikali ya kijiji ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo,” amsema Njiro.

Afisa Uhusiano wa Huduma kwa Wateja TANESCO Ruvuma, Allan Njiro akitoa elimu kwa wananchi wa vitongoji vya Matemanga na Mkurusi vilivyopo katika kata ya Kigonsera Halmashauri ya Mbinga vijijini, ambapo aliwatahadharisha dhidi ya matapeli wanaowatoa fedha nyingi kwa ajili ya kuunganisha umeme kinyume na utaratibu wa shirika hili.

Hata hivyo, amewaeleza wananchi kuwa Serikali iimeleta Mradi wa Ujazilizi, ambao baadhi ya vijiji vinakuwa na umeme, lakini kuna maeneo hayajafikiwa na huduma hiyo hivyo wanahakikisha wanapatiwa umeme.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kigonsera, Simon Komba amwataka wananchi wa vitongoji hivyo kutoa ushirikiano kwa TANESCO pindi mradi huo utakapoanza ili waweze kumaliza kwa wakati.