Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
IKIWA ni muendelezo wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeendelea kuwashukuru wateja wake wakiwemo makampuni ya utalii, wawekezaji na jamii kwa ujumla.
Shukrani hizo zimewaendea ambao wameendelea kuwa msingi wa uhifadhi na mapato kwa ajili ya kuimarisha miundombinu mbalimbali ndani ya taasisi na Taifa kwa ujumla.
Kutokana na umuhimu wa wiki hii, Oktoba 8, 2025, Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Rubondo imepokea wananchi zaidi ya 40.

Wananchi hao ni miongoni mwa wateja wake wakuu waliojielekeza kufanya utalii wa ndani na kupata elimu ya uhifadhi wa maliasili ikiwemo ulinzi wa mazalia ya samaki.
Aidha, Wananchi hao ni kutoka katika kata tatu za wilaya ya Chato ambazo ni Muganza, Bwongera na Kigongo.
Mbali na kufanya utalii wa ndani na kupata elimu ya uhifadhi pia ziara hiyo ilijikita zaidi katika kuimarisha mahusiano kati ya hifadhi na jamii zilizoko pembezoni mwa hifadhi hiyo.
Lakini pia, kujadili njia bora za kukuza ushirikiano uliopo baina ya pande hizo mbili ili kufikia lengo la uhifadhi endelevu wa maliasili na maendeleo ya jamii.



More Stories
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10