December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANAPA kukusanya sh.343 bil kipindi cha 2023/24

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

KAMISHINA wa Uhifadhi za za Taifa (TANAPA) William Mwakilema mwelekeo wa Shirika hilo kwa mwaka 2023/24 ni kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 343.8 kutoka vyanzo vya ndani vya mapato huku likiwa na matarajio ya kupokea wageni milioni 1.8.

Mwakilema ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Taasisi hiyo kwa mwaka 2023/24 jijini Dodoma huku akisema Shirika hilo linatarajia kuwezesha shughuli mbalimbali kwa gharama ya shilibgi bilioni 118.3 pamoja na shilingi bilioni 60 .6 kutekeleza miradi ya maendeleo.

Aidha Kamishna huyo wa Uhifadhi amesema,Shirika hilo litawezeshwa fedha shilingi bilioni 194 kupitia mradi wa Regrow na KfW ili kuchangia bajeti hiyo ya shirika hasa katika miradi ya usimamizi ,ulinzi na miundombinu ya Utalii.

Kwa mujibu wa Kamishna huyo wa Uhifadhi ,katika kuboresha mahusiano mema na wananchi waishio pembezoni mwa hifadhi ,shirika litachangia shilingi bilioni 2.3 katika miradi ya maendeleo ya jamii 23 zilizopo katika wilaya za Bagamoyo,Chato ,Hai,Kondoa,Kaliua,Korogwe,Karatu ,Kyerwa ,Liwale ,Moshi Vijijini ,Muleba,Rifiji,Siha,Tarime na Urambo.

“Kkwa ujumla Shirika litatoa kipaumbele katika maeneo ya Uhifadhi ,ulinzi ,Utalii,ushirikishaji jamii,uboreshaji miundombinu,teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na kuimarisha rasilimali watu.”amesema Mwakilema

Aidha ametaja maeneo mengine yaliyozingatiwa kuwa ni pamoja na ukamilishaji wa miradi ya kimkakati na miradi maendeleo ya shirika ambayo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji huku akisema shirika la TANAPA litatekeleza mipango ya masuala mtambuka ikijumuisha hifadhi ya mazingira ,mabadiliko ya tabianchi ,makundi maalum ,vita dhidi ya ukimwi na magonjwa yasiyo ya kuambukza na Utawala Bora.

Akizungumza kuhusu mikakati ya TANAPA amesema ni pamoja na kuendelea kuhifadhi wanyamapori ,bioanuai na makazi ya wanyama katika hifadhi za Taifa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo,kuongeza kasi ya matumizi ya sayansi na teknolojia katika uhifadhi hususan kulinda viumbe asimu na walio hatarini kutoweka ili kuhakikisha idadi yao inaongezeka kwa asilimia 10 hadi ufikia Juni 2026.

Makilema ametaja mikakati mingine kuwa ni kutumia teknolojia katika kupambana na ujangili ,kuimarisha shughuli za Intelejensia na upelelezi na kuongeza kasi ya utoaji elimu yauhifadhi kwa jamii.