Na Mwandishi wetu,Timesmajira
CHAMA Cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) imezindua makala inayoangazia elimu bora na elimu jumuishi kwa watoto walio hatarini kuacha shule .
Makala hiyo iliyoandaliwa na chama hicho kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali la We World imelenga kuamasisha upatikanaji wa elimu bora na jumuishi Kwa watoto.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo Septemba 23, 2024,Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA ,Dkt Rose Reuben Meneja Miradi Mkakati (TAMWA) Sylvia Daulinga .
Amesema makala waliyoiandaa imeleta pamoja sauti za watoto, wazazi, walimu, mashirika na ofisa wa serikali ambao wamefunguka kuhusu jinsi ya kuvunja vikwazo vinavyowazuia watoto kupata elimu bora na sio bora elimu pamoja na kusisitiza haja ya haraka ya kukabiliana na changamoto kupitia uwezeshaji wa jamii, ushirikiano na kuboresha sera za elimu nchini.
“Makala hii inasisitiza haja ya sera na mikakati inayolenga kusaidia makundi hatarishi kama vile wasichana, watoto wenye ulemavu, watoto kutoka familia masikini na kutoka kwenye jamii zilizo pembezoni kwa kuboresha mazingira ya shule wanaweza kufanikisha elimu bora na watoto kufurahia kwenda shule,” amesema
Vilevile amesema makala hiyo imeleta pamoja sauti za watoto, wazazi, walimu,Mashirika ya kiraia na Ofisa wa Serikali ikiazisha mazungumzi kuhusu jinsi ya kuvunja vikwazo vinavyowazuia watoto kupata elimu bora na sio bora elimu.
“Makala hii inasisitiza haya ya haraka ya kukabiliana na chagamoto hizi kupitia uwezeshaji wa jamii, ushirikiano na watu wenye ushawishi na kuboresha sera za elimu nchini”amesema
Aidha amesema mradi huo umejikita katika maeneo ya Dar es salaam ambapo jumla ya walimu 200 wanatarajia kufikiwa.
Pia ameongeza kuwa mradi huo ni wa kipindi cha miezi sita huku ukitegemea kuwa chachu ya kuanzisha mazungumzo hususani katika shule za umma na Serikali.
More Stories
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25