
MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya huduma za Maktaba Nchini Mboni Ruzegea amesema bodi hiyo imejipanga kukagua maktaba zote nchini na kuweka miongozo itakayosaidia udhibiti wa majarida na machapisho yasiyofuata maadili ya kitanzania hasa yanayoingia nchini kutoka nje ya nchi kama misaada.
Ruzegea amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya namna majarida na machapisho yanayosambazwa ndani ya jamii yanavyohatarisha uvunjifu wa maadili nchini na kutoa wito kwa waandishi wa majarida na vitabu kutosambaza kazi zao mpaka kazi zao zihaririwe na bodi hiyo iliyopewa kazi hiyo kisheria.
Kauli hiyo ya Mkurugenzi Mkuu wa huduma za maktaba inakuja baada ya kubainika kwa Taasisi ya Athuman Kapuya mkoani Tabora kusambaza vitabu vinavyofundisha mapenzi ya jinsia moja ndani ya jamii hasa kwenye shule mbalimbali mkoani Tabora.
More Stories
Kanisa la Shincheonji la Yesu nchini Ufaransa lakanusha ripoti ya Le Parisie
Vyombo vya ulinzi na usalama Mbeya,Benki kuu kushirikiana kutatua changamoto za utapeli mtandaoni
Polisi Mbeya kuimarisha ulinzi kuelekea sikukuu ya Pasaka