January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tamasha la Rejoice Tanzania kufanyika viwanja vya Uhuru

Na Jackline Martin

Kanisa la Moravian jimbo la Mashariki wameandaa tamasha liitwalo rejoice Tanzania litakalofanyika Septemba 16, 2022 lengo ni kumsifu mungu, kuliombea Taifa la Tanzania na kuisaidia jamii kutatua changamoto mbalimbali

Katika Tamasha hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye

Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa Moravian Efatha Choir, Judith Joram alisema tamasha hilo litakua siku ya Ijumaa katika uwanja wa Uhuru na litaanza usiku na kuisha asubuhi;

“Katika tamasha hilo tutatangaza injili ndani na nje ya nchi lakini pia pesa zitakazopatikana katika tamasha hilo tutakuwa na fungu la kumi ambalo litaenda kuisaidia jamii kutatua changamoto mbalimbali”

Aidha alisema katika tamasha hilo kutakuwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ikiwemo Congo, South Afrika n.k, ambao ni waimbaji wa Choir mbalimbali na binafsi.

Pia Judith alisema katika Rejoice Tanzania Balozi wao atakua ni Mchungaji Emmanueli Mgaya (Masanja)

Kuhusu Tiketi, Judithi alisema zitapatikana kwa shilingi 15,000 , 20,000 , 50,000 , 500,000 na 1, 000, 000

Pia Tisheti zitapatikana kwa shilingi 15,000 , 20,000 na 25,000
Aidha Judith alisema Tamasha hilo lilianza tangu mwaka 2019 na litakua endelevu.

Kwa upande wake Balozi wa Tamasha hilo, Emmanueli Mgaya (Masanja) alisema siku hiyo itakuwa ni ya tiba kwani utatibiwa kiroho hii ni kutokana na Choir zitakazoimbwa siku hiyo pamoja na maombi yatakayoombwa.

Kwa upande wake Mlezi wa Kanisa hilo aliwakaribiwa wananchi wote kutokukosa tamasha hilo kwani litakuwa ni la kushukuru, kusifu na kupata baraka