Na Bakari Lulela, TimesMajira Online
TASNIA ya sanaa Leo Septemba 7, 2024 wanafanya Dua maalum ya kuwakumbuka wapendwa wao waliotangulia mbele ya haki kutokana na michango yao dhidi ya kazi zao.
Akizungumza jijini Dar es salaam katika viwanja vya Leaders Suzana Lewis maarufu Natasha amesema waliotangulia wameacha mapengo mengi ambayo hayawezo kuzibika.
Amesema wasanii waliotangulia mbele ya haki wote anawakumbuka kwa kazi zao namna alivyogusa jamii kwa ujumla.
“Tutaendelea kuwakumbuka kwa kazi walizozifanya kuwaenzi ni jambo kubwa sana kulingana na kitu walichokifanya,” amesema,” Natasha
Amesema inauma sana Kuna watu wameondoka wakiwa wadogo sana na wengine wakubwa tulikuwa nao karibu lakini wameacha pengo.kubwa sana.
Msanii huyo aliwataja baadhi ya wasanii waliotangulia mbele ya haki ni pamoja na Kanumba,Maunda Zolo na Amina Chifupa ambaye alikuwa rafiki yake mkubwa.
pia amesema wao kama wasanii waliobaki wataweza kukumbukwa kama wenzao wanavyokumbukwa na je vipaji vyao tunavitumia ipasavyo,”amesema.
More Stories
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa