Na Heri Shaaban , TimesMajira Online
TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Ilala yaokoa shilingi bilioni 3.2 kwa kipindi cha Julai hadi September kwa kushirikiana na Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ikiwa ni makusanyo mbalimbali ambayo hayakuwasilishwa Benki kwa muda mrefu.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala Sosthenes Kibwengo , aliwataka wote wanaokusanya na kusimamia mapato ya Serikali kuwa matumizi ya fedha mbichi yameharamishwa na jinai haifi hivyo wazingatie taratibu za makusanyo na matumizi ya fedha za Umma.
“TAKUKURU Mkoa wa Ilala kwa kipindi cha miezi mitatu Julai hadi September tumefanikiwa kuokoa shilingi bilioni 3,244,449,921 makusanyo mbalimbali ambayo hayakuwasilishwa benki na wakandarasi kwa kipindi hicho cha robo ya tatu “alisema Kibwengo.
Mkuu wa Takukuru Ilala Kibwengo alisema pia katika miradi ya maendeleo 11 ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Takukuru Ilala wameokoa shilingi bilioni 10.4 pesa hizo walizookoa katika sekta ya ujenzi, Sekta ya Elimu na Barabara ili kubaini na kuzuia uchepuzi wa vifaa na ucheleweshaji wa miradi na kukuza ushirikishwaji wa Jamii pamoja na upatikanaji wa thamani ya fedha.
Aidha alisema katika miradi mikubwa ya maendeleo imebainika kasoro zikiwemo kutozingatiwa kwa mikataba hasa matakwa ya ujenzi na kughushiwa kwa taarifa za vipimo vya ubora wa vifaa vya ujenzi pamoja na kasoro kurekebishwa ambapo wameanzisha uchunguzi kwenye mradi mmoja wa Shule ya Msingi Kidole Kata ya Msongola wenye thamani ya shilingi milioni 80 baada kubaini udanganyifu wake katika utekelezaji wa mradi huo.
Wakati huo huo TAKUKURU mkoa wa Ilala wamefanya chambuzi mbili mfumo wa Mapato soko la Ilala Boma wamebaini kiasi chote cha kodi iliyozuiwa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na wakati mwingine kuchelewa kuwasilisha.
“Katika soko la Ilala Boma tumebaini kupotea kwa mapato mengi kutokana na rekodi potofu ya idadi ya wafanyabishara ambapo wakati mwingine uhalisia wa idadi ni mara mbili au hata zaidi ya ile inayosemwa na kutumika kukadiria kodi na tozo mbalimbali.
Alisema wamefanya vikao kazi na wadau wa idara ya mapato na Barabara na kuwasilisha taarifa za uchambuzi ufatiliaji ,kuzijadili,na kukubariana na maazimio ya kuboresha mapungufu yaliobainika katika chambuzi za mfumo na ufatiliaji wa miradi ya maendeleo.
Taarifa kamili inaendelea usikose toleo la kesho na
Mwandishi wako Heri shaaban Mzalendo
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua