Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Mbeya
TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa(PCCB) mkoa wa Mbeya imesema kuwa katika kipindi cha uchaguzi ngazi ya chama na jumuiya taasisi hiyo ilishiriki kufuatilia mchakato wote kuanzia ngazi ya`kata mpaka mkoa na kubaini mmoja wa wagombea wa uchaguzi wa mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC)kushiriki vitendo vya rushwa na uchaguzi huo kusimamishwa.
Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mbeya ,Maghela Ndimbo amesema hayo leo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya utendaji kazi wa ofisi ya Takukuru kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Mwezi Julai mpaka Septemba 2022 kuhusiana na miradi ya maendeleo 32 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bil.11.1 ambayo inafuatiliwa.
Mkuu huyo wa Takukuru Ndimbo amesema kuwa katika kipindi cha harakati za uchaguzi kunakuwa na mambo mengi hivyo Takukuru ilishiriki kufuatilia ngazi ya kata mpaka mkoa na jukumu kubwa la taasisi hiyo ni kubaini rushwa na kuzuia.
“Pale wanapobaini mgombea yeyote ambaye yupo kwenye mchakato wa uchaguzi wanakishauri chama kumwondoa mgombea kushiriki uchaguzi na hatua nyingi zilifanyika kwa mchakato huo na wengi waliohusishwa na vitendo hivyo waliondolewa kushiriki na kusema kwenye levo ya mkoa walibaini mmoja wa washiriki wa wagombea wa mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) alikuwa anashiriki vitendo hivyo vya rushwa lakini kwa kutumia mfumo wetu tuna kitengo cha Interejensia walibaini kwenye mfumo huo kuwa mgombea huyo alikuwa anakusanya watu nyumbani kwake na kugawa fedha kama nauli kitendo ambacho ilikuwa kinyume cha tarabu cha chama “amesema Mkuu huyo wa Takukuru.
Akielezea zaidi Mkuu huyo wa amesema fedha hizo waliweza kuzuia kwenda kwa wajumbe ambazo zilikuwa kwa wakala wake hivyo kwasasa suala hilo limezuiwa na ndomana uchaguzi huo umesimamishwa hivyo wanatusubiri chama kitachukua hatua gani.
Aidha Mkuu huyo Takukuru Ndimbo amesema kuwa wameshirikiana na chama vizuri kwa wale wote walioshiriki vitendo vya rushwa wengi wao waliondolewa hasa waliogombea ngazi ya wilaya na mkoa kuanzia chama na jumuiya zake na kusema kwamba matukio mengi yaliyotokea kwenye uchaguzi yapo kwenye uchunguzi .
Amesema kuwa hatua zinazochukuliwa ni kwamba mtu akibainika hatakiwa kuwa kiongozi ,na vitendo kama ni vya uzuiaji na suala la mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa lipo kwenye uchunguzi zaidi na mkoa umekamilisha na kupeleka sehemu husika zaidi na yakitolewa maelezo ya kimahakama litafanyika .
Kwa Mujibu wa Kamanda wa Takukuru mkoa wa Mbeya, Ndimbo amesema kuwa wakala alikuwa anapewa fedha na muhusika ili agawe kwa wajumbe na kitendo cha wakala kupewa zile fedha agawe hakikufanyika .
Hata hivyo Ndimbo amesema kuwa Takukuru mkoa wa Mbeya imetekeleza kazi tatu za uzuiaji wa rushwa ambazo ni ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ambayo ni matumizi ya fedha za mpango wa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19 na uchambuzi wa mifumo.
Ndimbo amesema kuwa pia Takukuru iliweza kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo 32 yenye thamani ya shilingi Bil.11 lengo likiwa ni kufuatilia miradi ili kuhakikisha kuwa miradi yote inatekelezwa kwa ubora uliokusudiwa na kwa thamani halisi ya fedha iliyotolewa na kutumika na pia kuhakikisha utekelezaji wa miradi unakamilika ndani ya muda uliopangwa ili wananchi wapate huduma iliyokusudiwa na`serikali.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua