Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imetoa ufafanuzi namna ambavyo teknolojia ya Nyuklia inavyoboresha Sekta za kilimo, mifugo na rasilimali za maji hapa mchini.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengp cha Mawasiliano wa Tume ya Nguvu za Atomic Tanzania (TAEC) jijini Mbeya katika maonyesho ya wakulima Nane Nane.
Amesema, teknolojia hiyo ya nyuklia hutumika kuboresha mazao ya Kilimo, Mifugo sanjari na utafutaji na uboreshaji wa rasilimali ya maji.
“Matumizi ya Teknolojia ya Nyuklia duninai ni makubwa na teknolojia hii imekuwa mkombozi katika kutokomeza wadudu waharibifu katika mazao yatokanayo na kilimo na mifugo, hivyo kupunguza kuenea kwa wadudu na magonjwa, kuongeza uzalishaji wa mazao, kulinda rasilimali za ardhi na maji, kuhakikisha usalama wa chakula na kuongeza uzalishaji wa mifugo.” amefafanua Ngamilo na kuongheza kuwa
“Shirika la Chakula Duniani (FAO) na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) ambapo Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ni wanachama wamekuwa wakipanua maarifa na kuongeza uwezo katika eneo hili kwa zaidi ya miaka 50 na matokeo na mafanikio makubwa yanaonekana ulimwenguni kote kupitia teknolojia hii.”
Akiainisha baadhi ya mifano jinsi Teknolojia ya Nyuklia inavyoboresha kilimo na mifugo katika nchi wanachama wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani Ngamilo amesema,ni katika uzalishaji wa wanyama na uboreshaji wa afya za mifugo, Uboreshaji wa udongo na maji, Usimamizi wa Wadudu na Usimamizi wa Wadudu.
“Katika uzalishaji wa wanyama na uboreshaji wa afya za mifugo Teknolojia ya Nyuklia hutumika na kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta za kilimo na mifugo katika kuongeza uzalishaji wa mifugo, kudhibiti na kuzuia magonjwa mtambuka ya wanyama na kulinda mazingira,” amesema Bw. Ngamilo.
More Stories
Serikali yaja na mwarobaini wa changamoto ya Kivuko Magogoni – Kigamboni
Kisarawe kukata keki ya Birthday ya Rais Samia
Wataalam wa afya wakutana kujadili ugonjwa wa Marburg