January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TADB yatoa mafunzo ya kilimo kwa Viziwi

Na Penina Malundo, Timesmajira

Jamii imeshauriwa kutambua na kuthamini kundi Maalum la Viziwi katika kuwashirikisha katika uchumi jumuiashi ili kusaidia kuondokana utegemezi kwani nao wananguvu na wanaweza kufanya kama watu wengine ili waondokane na amasikini.

Ushauri huo umetolewa leo Mkoani Morogoro na Afisa Tawala Ofisi ya Wilaya ya Morogoro,Hilary Sagara wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya siku tatu kwa wakulima na wafugaji wenye uviziwi yaliyoandaliwa na Benki ya Kilimo Maendeleo Tanzania (TADB) lengo ni kuwajengea uwezo wa nadharia na vitendo Viziwi ili waweze kulima na kufuga kwa namna bora na iwasadie kuwainua kiuchumi .

Hata hivyo amesema kundi hili limekuwa likipitia changamoto mbalimbali ikiwemo ya kutokusikia hivyo Jamii imekuwa ikiwasahau katika kuwashirikisha katika kufursa mbalimbali ikiwemo katika sekta ya kilimo.

Amesema benki ya TADB ni ya serikali imeonesha mfano kwa kampuni na taasisi mbalimbali kuiga kuwasaidia licha ya changamoto waliyo nayo lakini wananguvu za kufanya kazi na kujipatia kipato .

“Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassani imejipanga vizuri hivyo kila halmashauri zote Nchini zimepewa kiasi cha asilimia mbili cha fedha kwa ajili ya kukopesha makundi Maalumu ikiwemo walemavu viziwi bila riba yeyote hivyo nawasihi mjiunge katika makundi ili wapatiwe fedha hizo”amesema Sagara

Mwenyekiti Mtendaji Kituo Cha Wakulima na Wafugaji KIWAWAVITA Tanzania wa Habibu Mrope akizungumza katika mafunzo ya viziwi kuhusu masuala ya Kilimo.

Naye Afisa Biashara Mkuu Kanda ya Mashariki Kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania TADB Gryson Ferdimang amesema benki la Kilimo imeamua kusaidia Mafunzo hayo kwa kundi hilo kwani nao Wanaweza kufanya kazi isipokuwa tu kipato chao ni changamoto hivyo kupitia Mafunzo haya wataondoka wakiwa wamejipatia fursa nmna ya kuomba mikopo kupitia benki hiyo.

Naye Mwenyekiti Mtendaji Kituo Cha Wakulima na Wafugaji KIWAWAVITA Tanzania wa Habibu Mrope amesema wao viziwi wanapitia changamoto nyingi ikiwemo kutokuaminika katika makampuni mabenki kwa kukosa dhamana ya kuomba mikopo na kujieleza hivyo ni kwa mara ya kwanza benki ya TADB imewakubalia kuwapatia Mafunzo ya kwa nadharia na vitendo wanashukuru sana isiishie hapa wafuatiliwe na miradi yao wanayoifanya ikiwemo kilimo

Kwa upande wake mwezeshaji mada kutoka Tanzania Horticultural Association (TAHA) Elisha Mhomisoli amewashauri wanapoamua kulima Kilimo ikiwemo cha viungo,maua, mbogamboga,mbegu wahakikishe kuwa wanalima kisasa kwa kuhudumia vizuri na kuweka mbolea maji ya kutosha Ili wavune vizuri hivyo licha ya kuwepo na janga la ukame ambao umeikumba nchi hawana budi kukata tamaa kulima .