November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Taasisi ya ‘Who is Hussain’ kukusanya damu Arusha

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Taasisi ya who is Hussain kutokea mkoa wa Arusha inatarajia kufanya kambi maalumu ya ukusanyaji wa damu Kwa mkoa wa Arusha Ambapo Akiba ya damu ni muhimu Sana kwenye hospitali.

Akizungumza na vyombo vya habari mkurugenzi wa whoishossein kwa mkoa Arusha Tahera Abaisi alisema kuwa kambi hiyo inalenga kukusanya damu ambazo zitakuwa Akiba mahospitalini.

Tahera alisema kuwa Kwa sasa bado damu inahitajika Sana Kwa kuwa huwa kuna dharura kubwa ambazo zinatokea za maitaji ya damu na wakati mwingine huwa dharura hizo ni za haraka.

Alifafanua kuwa Akiba ya damu inapokuwepo inaweza kuraisisisha kuokoa maishaa ya wagonjwa na waitaji ambayo Nayo wakati mwingine huwa yanatokea kwa dharura.

Alitaja dharura hizo za mahutaji ya damu Katika mahospitali ni kwa makundi kama vile kwa wajawazito watoto,watu wazima,lakini hata waliopata uhitaji kutokana na ajali.

“Napenda sana kuwasihi watanzania kuhakikisha kuwa wanakuwa pamoja na Sisi na kuchangia damu salama ili akiba ya damu iwepo na ya kutoshaa “alisema Tahera.

Katika hatua nyingine alisema kuwa taasisi hiyo ya Whoishossin alisema kambi hiyo inatarajia kukusanya uniti nyingi zaidi ambapo Kwa mwaka Jana walikusanya kiasi cha uniti 486 za damu na iliweza kusaidia na kuokoa maisha ya watu 1486

Awali Mwakilishi wa taasisi hiyo mkoa wa Arusha Dkt Hamza Abbasi alisema kuwa kambi hizo zitakusanya damu lakini pia kabla ya hapo damu ambayo itakusanywa itaweza kupita katika mchakato wa usalama na upimaji wa ubora alisema kuwa watu wanapotoa damu unaweza kuwaraisishia hata kupata huduma ya haraka pindi uitaji unapokuwepo hivyo ni muhimu Sana Kwa watanzanja kuhakikisha kuwa wanachangia damu kwa wingi hususani Katika kambi hiyo ambayo inalenga ukusanyaji wa damu.

Alitaja kambi hizo kuwa zitafanyika katika shule ya sekondari mringa,mukulati sekondari,hospitali ya Kwa Dkt Mohamed, na July 29 wataweka kambi tena katika msikiti wa Aghakani pamoja na hospitali ya Mega Care njiro.

Dkt Hamza alimalizia kwa kuwahimiza hata Kwa wale ambao wapo mbali yaani vijijini nao wanaiweza kufika mjini na kuwasiliana na taasisi hiyo ambapo wataweza kugharamikiwa naitaji muhimu ili nao waweze kuchangia Akiba ya damu.