Na Bakari Lulela, TimesMajira Online
TAASISI isiyo ya kiserikali ya TuSe kimara jijini Dar es salaam, imeendesha mdahalo maalumu kwa wananchi kufahamu mahusiano yaliyopo katika ya serikali kuu na serikali za mitaa.
Hayo yamejili kwenye mdahalo uliowashirikisha baadhi ya viongozi na wananchi wa kawaida ambapo mgeni rasmi alikuwa katibu mwenezi wa CCM kimara Ahmed mursaly amesema taasisi zote zinafanya kazi kwa kutegemeana lakini zote lao ni moja kuwatumikia wananchi.
“Taasisi zote hizi zinafanya kazi pamoja ambayo ni ya kuwatumikia wananchi wa Tanzania pasi na kubagua ELIMU walizonazo, itikadi zao na rangi zao,” amesema Ahmed
Aidha Ahmed amesema kufuatia mdahalo kuwa na mchuano mkali wananchi walipewa angalizo kuwa kipindi hiki walichonacho ni mwaka 2024 tunaelekea uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo amewahimiza kushiriki katika zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi huo.
Hata hivyo amesema ifikapo mwaka 2025 tutakuwa katika zoezi la kuwachagua viongozi wa serikali kuu ambapo ni Raisi, mabunge na madiwani wa kada mbalimbali ambapo watakapata nafasi ya kuwatumikia wananchi kwa kipindi cha miaka mitano.
Kwa upande wake mwalimu Hamad Zongo ambaye alikuwa katika nafasi ya kuchochea mada amesema kinachoendelea hapo ni uelewa baina ya wananchi kufahamu mahusiano yaliyopo kati ya serikali kuu na serikali za mitaa.
Hivyo mwalimu Zongo amesema mdahalo huo umetoa dira kwa walio wengi kuweza kutambua. Mahusiano yaliyopo baina ya serikali kuu na serikali za mitaa ingawa serikali za mitaa zinaendesha vikao vyake vingi kwa kuwashirikisha wananchi
More Stories
TCC yaibuka kidedea tuzo za PMAYA
Mwanafunzi apoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba
Mwanafunzi adaiwa kuuwawa na rafiki wa baba yake