Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha
Taasisi ya Future STEM Business Leaders kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Arusha ( Arusha Technical College ) wameandaa na kutoa mafunzo ya siku nne kwa wanafunzi wa kidato cha tano na Sita katika Jiji la Arusha kutoka katika shule Saba zilizopo mkoani hapa
Akifungua mafunzo ya siku 4 kwa wanafunzi hao kaimu Mkurugenzi mtendaji wa atamizi ya DTBi Dkt Easton Mlyuka alisema kuwa bado kuna mambo hasa ya teknolojia ambayo yanatakiwa yafanyike ili taifa lizidi kukua kuanzia ngazi za chini
Alibainisha kuwa katika ustawi wa uchumi wa nchi ya Tanzania kuna wategemea wataalamu wetu wa ndani na kwa kupitia programu hiyo maalaum ya sayansi teknolojia na ubunifu itasaidia kuweza kuwapata
“Lengo halisi ni kuona kuwa haya mafunzo hayo yatasaidia sana kupata kizazi cha watafiti na wabunifu katika nyanja mbali mbali hapa nchini”ndio maana leo tumewakutanisha wanafunzi hawa
Alisema kuwa mradi huo ulianzia kwenye vituo vya kitaaluma ili kukuza mawazo na kuyapeleka katika ubunifu na pia kuyabadilisha na kuwa bidhaa na kisha kuyapeleka sokoni na kutumika kwenye jamii.
“Tulianza programu hii na shule 5 kwa mwaka 2019 na tulikuwa na wanafunzi 40 Mpaka sasa tunao wanafunzi 85 na shule 17 pia tulianzia jijini Dar es salaam lakini sasa tupo Arusha ambapo awali Kwa Arusha Tulianza na shule tano na Sasa tumeongeza mbili kwahiyo Kwa hapa Arusha tu tunashule Saba zilizopo katika programu hii “. Alisema Dk Mlyuka.
Alifafanua kuwa pindi unapokuwa na wazo lazima uwe na ubunifu kwa kile unacho kiona kwenye jamii ili kuweza kupata suluhisho ya jambo hilo, ambapo wazo hilo lazima liwe na manufaa kwa jamii na linatakiwa liwe na ubora wa ubunifu na kutoa matokeo chanya ambayo mwishowe litatumika na jamii kisha kuleta faida na kusaidia kutoa ajira pia ukiwa na wazo lazima uwe na upeo mkubwa wa kufikilia na uweze kulifanyia kazi kwa haraka.
Dkt Mlyuka alisema kwamba, ili kufanikisha ubunifu na kupata matokeo chanya kunatakiwa kuwe na ushirikishwaji wa wataalamu mbali mbali ambapo aliwataka wanafunzi hao kuwa wepesi katika kuomba ushirikiano kwa walimu wao pamoja na wataalamu walionao
kwa upande wake Meneja wa Mradi huo Josephine Sepeku, alisema kupitia mradi huo anaamini mafunzo hayo wataishi nayo kwa muda mrefu na yatatoa matokeo chanya katika masomo yao na yatapelekea kuwa wabunifu wazuri na wataalamu wazuri katika nchi.
Alisema madhumuni ya mradi huu hasa ni kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita na mradi huu wa sayansi ubunifu na biashara utawasaidia sana wanafunzi hao kuweza kukuza mawazo yao ya kisayansi kuyapeleka zaidi katika biashara
alibainisha kuwa taifa linaposema
Tanzania ya viwanda ili kuwe na viwanda lazima kuwe na wataalamu wa kutoka ndani ya nchi na ndiyo maana wameanza kwa kutoa mafunzo ya nadharia ili kuzidi kuwajengea uwezo toka wakiwa mashuleni.
Naye Kaimu Mkuu wa chuo cha Arusha Technical Dkt. Yusuph Mhando, alisema kwamba wamekuwa wakitoa mafunzo mbali mbali katika chuo cha ATC na wanafunzi wamekuwa ni bora zaidi na anategemea mafunzo hayo yatawajenga vyema katika elimu yao.
“Chuo chetu kimekuwa daraja bora kwa wanafunzi wote wanao pita hapa kwaajili ya kujifunza mambo mbali mbali hasa katika ufundi, ubunifu wa kisayansi kwakuwa nyie mmeonyesha dhamira nzuri ya kuwa sehemu ya kuendelea kujifunza nina imani kubwa sana mtakuwa sehemu ya mafanikio ya kupata wataalamu mbali mbali katika nchi yetu hasa katika maswala ya uwekezaji wa viwanda”. Alisema Dkt Muhando.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato