Na Rose Itono, TimesMajira, Online
WATANZANIA wameaswa kutumia chai ya asili inayotegenezwa na mimea ya asili ili kuuweza mwili kupata kinga sahihi na yenye virutubisho.
Akizungumza katika maonyesho ya 45 ya Kimatafa ya Biashara DTIF yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam, Mkurungezi wa Taasisi inayojishughulisha na utoaji wa tiba asili Cornewell Tanzania Elizabeth Lema, amesema unywaji wa chai ya asili iliyotegenezwa kiusahihi inamuwezesha mtumiaji kuimarisha kinga ya mwili.
Amesema kuna aina mbalimbali za chai ya asili ikiwepo Digestive te, Diabetes tea,Mango leaves tea,Giele Herbal tea, Eucalyptus Herbal tea na Cemon Leaves tea.
Aidha aliongeza mbali na chai kuna bidhaa nyingine ambazo zinatumia mimea ya asili kutibu magonjwa mbalimbali ambazo zimeboreshwa ili kukuwezesha mtumiaji kupata yenye usahih.
Aliwaasa watanzania kutembelea bada lao lililopo katika maonyesho hayo ili waweze kupata maelezo sahihi kutoka kwa wataalamu huku akiipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kutambua mchango wa tiba asili inayotokana na mimea.
“Naipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuthamini mchango wa tiba za asili na kusema kuwa wataendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha wanafanya kazi kwa usahihi ili kuimarisha afya za watanzania”amesema
Alisisitiza kuwa kuna magonjwa mengi ambayo yanaweza kutubika kupitia miti dawa.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi