Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
TAASISI ya Benjamin william Mkapa Foundation (BMF) kwa kushirikiana na Serikali imepanga kufanya jukwaa la kumbukizi ya pili ya kuenzi na kumkumbuka Rais Mstaafu, Hayati Benjamin Mkapa, litakalofanyika siku ya tarehe 13 – 14 julai 2022 katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tupil Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Juni 29, 2022, wakati wa kutambulisha kumbukizi ya pili, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Mkondya – Senkoro amesema kuwa Jukwaa hilo limepangwa kufanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, Zanzibar.
Mdahalo huo wa siku mbili utaanza saa Mbili asubuhi na unatarajia kumalizika saa nane mchana huku wageni waalikwa takriban 500 watahudhiria Siku ya kwanza mdahalo utafunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Othman Masoud.
Pia siku ya pili ya Julai 14,2022 itakuwa siku ya kilele cha mdahalo huo kwa mwaka 2022, na Mgeni rasmi katika siku hii muhimu atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
“Mdahala huu pamoja na mambo mengine utashirikisha jopo la wadau watakao chambua kwa undani umuhimu wa biashara ama uwekezaji wa pamoja katika kuinua afya na ustawi wa kila mmoja wetu.
“Hata hivyo Mdahalo huu wa siku mbili utaanza saa mbili asubui na unatarajia kumalizika saa nne mchana, Tunatarajia kuwa na wageni waalikwa takribani 500 siku ya kwanza ya mdahalo huo”, alisema Alisema, utafunguliwa na makamu mkuu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Othman Masoud na siku ya pili ya tarehe 14 julai itakuwa siku ya kilele cha mdahalo huu kwa mwaka 2022, na Mgeni rasmi katika siku hii muhimu atakuwa ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Samia Suluhu Hassan”.
Aidha viongozi wengine wa kitaifa watakaohudhuria mdahalo huu ni pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, Mh.Dkt Hussein Ali Mwinyi ambae pia ni msarifu wa Taasisi hiyo ambaye ni mrithi wa nafasi ya Hayati Benjamini Mkapa katika Taasisis yetu kuanzia Decemba 2021.
“Wageni wengine watakaoshiriki hafla hii ni pamoja na Viongozi wakuu wa Serikali, Marais na Viongozi wastaafu kutoka Tanzania Bara na Visiwani,Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa hapa Nchini Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Sekta binafsi za Umma, wanafamilia na marafiki wa Hayati Benjamini Mkapa kutoka ndani na Nje ya Nchi, pamoja na Asasi za kiraia na Viongozi wa dini. alisema na kuongeza,
Mbali na hayo, Katika siku hizo mbili kutakuwa na mdahalo kuhusu mada kuu mbili ambazo ni ambazo ni Kuongoeza kasi katika mikakati ya mabadiliko katika mifumo ya afya Tanzania kupitia biashara ushirika, (Accelerating Strategic Health Transformation in Tanzania through Business Coalition) na Ubunifu katika miradi na mikakati yaa ushirikiano kati ya Serikali, Taasisi za umma na za binafsi katika kuleta huduma ya afya kwa wote. (Innovative Public-Private Partnerships (PPP) approaches towards attaining Universal Health Coverage)
Kauli mbiu ya Jukwaa hilo ni “Uongozi Madhubuti Hamasa ya Mabadiliko kwa Wote.” (Resilient Leadership- Inspiring Change for All)
Dkt. Ellen alitoa shukrani kwa Wadau wote ambao wapo Pamoja nao katika maandalizi ya kufanikisha mdahalo huo wa kumbukumbu na kuenzi Maisha ya Hayati Mh. Benjamini William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamuhulri ya Muungano ya Tanzania na Msarifu wa Taasisi Benjamini william Mkapa.
More Stories
Chunya yafikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
HGWT yawarejesha kwao wasichana 88 waliokimbia ukeketaji
Sherehe Miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar zafana