Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inatarajia kufanya onesho la nane lijulikanalo kama Swahili International Tourism Expo( S!TE)litakalofanyika Oktoba 11 Hadi 13 ,2024 Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo Septemba 12,2024 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Ephraim Mafuru wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelezea uzinduzi wa Onesho hilo.
Aidha Mafuru amesema kuwa lengo la onesho hilo ni kuwakutanisha Watoa huduma waliopo katika mnyororo wa thamani wa Utalii Ndani na nje ya Nchi ambao watapata fursa ya kuonesha bidhaa zao za Utalii na kutengeneza Mtandao wa Biashara( Business Network)
” Onesho la S!TE linaenda sambamba na Utekelezaji wa sera ya Taifa ya Utalii ya Mwaka 1999 pamoja na mkakati wa kutangaza Utalii Kimataifa ( 2020-2025 ) ambayo imetilia mkazo kutangaza Tanzania kama kivutiok Bora Cha Utalii Duniani” amesema.
Nakuongeza kuwa “Onesho hili pia ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka mitano lll ( FYDP lll 2021/22-2025/26, ambapo zao la Utalii wa Mikutano na Matukio ( MICE Tourism) limeanishwa kama zao la Utalii la kimkakati kwa lengo la kufikia watalii milioni tano na mapato ya Dola za Marekani bilioni sita ifikapo Mwaka 2025.
Aidha ameendelea kusema kuwa Onesho hilo la nane la S!TE limebeba ujumbe usemao ” Explore Tanzania for a Life Time Investment and Seamless Tourism Experience” ambapo onesho hilo litahudhiliwa na waoneshaji wa bidhaa na huduma za Utalii zaidi ya 120 sambamba na wanunuzi wa bidhaa na huduma za Utalii ( International Hostel Buyers) takribani 120 kutoka Nchi ambazo ni masoko ya Kimkakati ya Utalii wetu ikiwemo Ulaya,Asia na Amerika.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TTB amefafanua kuwa Onesho hilo litafuatiwa na ziara za mafunzo ((FAM trips) ambazo zinalenga kuwajengea uelewa wahudumu wa bidhaa za Utalii kuhusu vivutio vya Utalii vilivyopo Tanzania ili waweze kuvitangaza katika Nchi zao na dunia kwa ujumla.
” Mwaka huu ziara hizo zimejikita katika kufungua Kanda za Utalii zinazochipukia ikiwemo ukanda wa Utalii Magharibi ( Western Circuit) na Ukanda wa Utalii Kusini ( Southern Circuit) na kufungamanisha shughuli za Utalii zinazofanyika Zanzibar na Tanzania Bara.” amesema Mafuru.
Amemaliza kwa Kuwaomba Watanzania na Vyombo vya habari kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha na kutangaza onesho la S!TE 2024 kwa lengo la kuwafikia Wadau wengi zaidi Ndani na nje ya Nchi ili waweze kunufaika na fursa za onesho hilo.
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo