Na Esther Macha,Timesmajira,Online,Mbeya
TAASISI ya Tulia trust inayoongozwa na Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson imekabidhi tani nne za vyakula kwa waislam kwa ajili ya kusherekea sikuu ya Eid El Fitr.
Pamoja na kutoa msaada huo pia amezifikia familia zenye mahitaji maalum wakiwemo wajane ,wazee pamoja na familia zisizojiweza mkoani Mbeya.
Msaada huo ulikabidhiwa leo katika Msikiti Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya Spika wa Bunge, Ofisa wa Taasisi ya Tulia Trust, Kapuya Athumani ,amesema kuwa mahitaji hayo ni sehemu ya maono ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya kwa kila mwaka kutoa kwa madhehebu ya dini.
Aidha Athuman ametaja vyakula vilivyokabidhiwa kuwa ni unga wa ngano,Mchele,Tende na mahitaji mengine mbalimbali kwa ajili ya waislam mkoani Mbeya na watu wenye mahitaji katika kusherekea Sikukuu hiyo .
Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ,Ayasi Njalambaha amesema kuwa kama waislam wanamuunga Mkono Spika wa Bunge kutokana na jinsi alivyojenga mahusiano mazuri na viongozi wa dini,jamii,pasipo kujali udini na pia wanamumbea dua Mungu amuondolee mabalaa.
Ameleeza kuwa waumini wa dini ya kiisalm wanatambua mchango mkubwa wa Spika wa Bunge hivyo watazidi kumwombea katika kazi zake ili aweze kufanya vizuri.
”Tunamuombea Dua Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya ,Dkt .Tulia Ackson Mungu amuepushe na mabalaa yoyote,katika usiku mzito wa kufikia siku ya Eid siku ambayo ni muhimu kwa waislam nchini Mei 3,mwaka huu”amesema.
Amesema kuwa wanaona na kutambua mambo makubwa yanayofanywa na Dk. Tulia hivyo wanamuombe heri Mwenyezi Mungu afanyie njia ya wepesi katika kuwatumikia wananchi na kushirikiana vyema na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuliongoza Taifa la Tanzania.
Njalambaha amesema kuwa katika kuelekea hiyo wanaliombea Taifa la Tanzania liendelee kudumisha amani,utulivu na viongozi wake wa ngazi zote Mora aweze kuwaongoza katika kufanya kila yaliyo ya heri kwa Watanzania pasipo ubaguzi wala itikadi za kisiasa.
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto