December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sirro aridhishwa na zoezi la uwekaji alama za mipaka Loliondo

Na Mwandishi wetu,timesmajira,Loliondo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro leo amefanya ziara katika eneo la Loliondo, Ngorongoro kwa ajili ya kujionea zoezi linaloendelea la uwekaji alama za mipaka, ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na kasi iliyopo.

IGP Sirro ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella, amewataka washiriki wa zoezi hilo kujituma ili kazi ya uwekaji alama za mipaka katika eneo hilo iishe kwa wakati.

Sirro amesisitiza wananchi kuwa watulivu na kushirikiana na serikali katika uamuzi huu wenye lengo la kuhifadhi eneo hilo kwa faida mtambuka za nchi.

‘Msikubali kutumika kuchochea vurugu ambazo hazina manufaa kwa pande zote na wala msikubali kutumika kwa niaba ya wale wote wasiotutakia mema kama taifa’, amesema Sirro.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha John
Mongella amemuhakikishia IGP Sirro kuwa Serikali ya Mkoa wa Arusha imejipanga kuhakikisha kuwa zoezi linaendeshwa kwa hali ya utulivu kwa kuzingatia sheria za nchi