Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo amewataka viongozi wa dini nchini Tanzania kuendelea kukemea vitendo vya ukiukwaji wa maadili katika jamii na visivyoendana na neno la Mungu ili kulinda mila na desturi nzuri za nchi yetu na kujenga taifa lenye upendo na amani
Sillo amesema hayo katika Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 150 ya Utume Ulimwenguni yaliyofanyika katika kanisa la Waadventista wa Sabato (SDA ) lililopo Mamba Myamba wilayani Same, mkoani Kilimanjaro leo Agosti 29, 2024
Amesema kuwa viongozi wa dini wanatakiwa kujihusisha katika kuendelea kulinda amani ya nchi yetu na kufanya amani ya nchi kuwa jambo la kwanza
“Ikiwa tunawafundisha watu kumtii Mungu ambaye ni chanzo cha amani ya kweli basi tunapaswa kuwafundisha waumini umuhimu wa kuendelea kuilinda amani”. Amesema
Aidha Sillo alitumia nafasi hiyo kuwahamasisha Wananchi kuwa Mwaka huu mwezi Novemba kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kuhuisha taarifa zao katika daftari la Wapiga kura
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Waadvestista Wasabato Jimbo kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Mark Malekana ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ushirikiano mzuri wanaoutoa kwa viongozi wa dini, aliongeza kuwa kanisa litaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali katika masuala ya Ustawi wa Jamii ili amani iendelee kutamalaki na kujenga taifa lenye ustawi.
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari