Na Tiganya Vincent,TimesMajira Online. Sikonge
HALMASHAURI ya Wilaya ya Sikonge, imetakiwa kuhakiki na kupima mashamba ya wanavijiji ambayo hayajapimwa, ili waweze kupatiwa hati ya hakimiliki ya kimila kwa ajili ya kuyaongezea thamani.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Peres Magiri wakati akikabidhi hati ya hakimiliki ya kimila za awamu ya pili 224 kwa vijiji vitatu na hivyo kufikisha hati 856, ambazo zimekwishatolewa chini Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).
Amesema hatua hiyo itasaidia kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi, ambao utasaidia kuondoa migogoro miongoni mwa wanavijiji wao kwa wao.
Magiri amesema Wilaya ya Sikonge, ina vijiji 71 lakini ambavyo wakazi wamepimiwa maeneo yao ni 12 na kubaki 59, jambo ambalo linahitaji kufanyia kazi ili kukamilisha vyote.
Mkuu huyo wa Wilaya, ameutaka uongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanatatua tatizo la mwingiliano wa maeneo 102 katika Vijiji vya Ukondamoyo, Mole na Usanganya ambalo ulisababisha MKURABITA, washindwe kuandaa hati za hakimiliki za kimila kwa wananchi.
More Stories
KNOCK OUT ya Mama Msimu wa tatu kufanyika Februari 28
CCM yaombwa kuchunguza vitendo vinavyofanywa na Mwenyekiti wa CCM Rorya
Rais Samia ataka watumishi kumaliza adha ya maji kwa wananchi