Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Shule ya Sekondari ya Zanaki Wilayani Ilala, inatarajia kufunga kamera za Usalama katika shule hiyo kila darasa kwa ajili ya kurahisisha ufanyaji kazi za Walimu shuleni hapo.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa shule hiyo Dellvene Koka ,wakati wa kupokea msaada wa kompyuta za kisasa kwa ajili ya kufunga katika chumba cha TEHAMA cha shule hiyo ambapo amesema kumpyuta hizo walizopewa wanajivunia katika kipindi hichi cha Dunia ya utandawazi ya Sayansi na Teknolojia.
“Tunapongeza wadau wa Elimu tasisi ya Power ComputersTehama kwa wote kuunga mkono Juhudi za Serikali katika sekta ya elimu leo tumepokea vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya kufundishia matumizi ya TEHAMA katika shule ya sekondari Zanaki “amesema Koka .
Mkuu wa Zanaki Mwalimu Koka, amesema mikakati ya shule hiyo kufunga kamera za usalama kwa ajili ya Mazingira ya shule pamoja na madarasani Ili Walimu waweze kufanya kazi zao kwa urahisi wakati wote mpaka kipindi cha mitihani ya ya majaribio na mitihani ya Taifa .
Koka amesema vifaa hivyo wa TEHAMA kwa wote watatumia vizuri na kuvitunza kwa ajili ya matumizi ya shule ya Zanaki sekondari .
Amesema mikakati mingine ya shule ya sekondari ya Zanaki Walimu wa shule hiyo kuwafungia kivaa Maalum kitakachokuwa kinapokea taarifa za Walimu wakati wa kuingia na kutoka kila Mwalimu awe anabofya shuleni hapo kwa ajili ya kufatilia maudhurio yao wakati wa kuingia na kutoka .
Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji Pili Radhidi, amepongeza wadau wa Elimu TEHAMA kwa wote kwa msaada huo waliopokea katika kuunga mkono sekta ya Elimu kusaidia Serikali.
Afisa Elimu Pili Radhidi amesema Teknolojia hiyo itawafanya Shule ya Zanaki iwe ya kisasa katika nyanja za Saysnsi na Teknolojia .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Power computers Telecommunication Ltd Shakil Dharamsi amesema ameamua kuwekeza sekta ya elimu katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika Sekta ya Elimu ambapo mfumo huo wa TEHAMA waliofunga shule ya sekondari ya Zanaki utawasaidia Wanafunzi wa shule hiyo na Watanzania kwa ujumla kwani kila kitu kipo TEHAMA .
Mkurugenzi wa TEHAMA kwa wote Shakil amesema kampeni hiyo ya kufungua mfumo wa TEHAMA shule za Serikali ni endelevu zanaki ni shule ya tano kufunga mfumo huo , wakipata tena wafadhili watafunga shule nyingine.
Katibu wa TEHAMA kwa wote Evelin Malamsha amesema imeshatoa elimu kwa Walimu kujifunza Maswala ya TEHAMA dhumuni lao Walimu wa shule ya Zanaki kuwawezesha pia kujifunza TEHAMA.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba