January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule ya Sekondari Zanaki wajivunia mafanikio, ufaulu waongezeka

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

SHULE ya Sekondari Zanaki wilayani Ilala wajivunia mafanikio kitaaluma inafanya vizuri katika matokeo ya miaka mitatu imefanya vizuri imeshika alama za juu kidato cha sita .

Akizungumza katika mahafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Zanaki, Mkuu wa Shule hiyo Dellvine Koka ,alisema katika kipindi cha miaka mitatu wanafunzi wamefaulu kwa asilimia 100 ,mwaka 2021 asilimia 100 mwaka 2022 asilimia 100 mwaka 2023 asilimia 98.65.

“Tunajivunia ufaulu wa miaka mitatu mfurulizo katika shule yetu tumefanya vizuri jitihada za walimu wangu na wanafunzi ambapo wanafunzi wamepata daraja la kwanza mpaka la tatu “alisema Dellvine.

Mkuu wa shule hiyo Dellvine Koka, alisema mwaka 2024 jumla ya wanafunzi 181 wa kidato cha sita wanatarajia kufanya mitihani yao hivi karibuni wanafunzi hao wameandaliwa vizuri kitaaluma na walimu wao wana imani watafanya vizuri katika mitihani hiyo

Aidha alisema mikakati ya shule hiyo Walimu na wanafunzi wameweka mpango wa kuondoa daraja la nne na safari ambapo juhudi walionyesha katika Mitihani ya majaribio Mock na Pre National ni dhairi kuwa wataenda kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa NECTA .

Akizungumzia historia ya shule ya Sekondari Zanaki ni miongoni mwa shule kongwe hapa nchini Tanzania ilianzishwa mwaka 1939 kwa jina la Agha Khan ,baadae Serikali walichukua na kubadirisha jina kuitwa Zanaki Sekondari mwaka 1970 shule ina wanafunzi 1,050 wa kidato cha kwanza mpaka cha sita walimu 58,watanzania na mmoja kutoka China,walimu wa kujitolea sita .

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Diwani wa Kata ya Upanga MASHARIKI Sultan Salim ,kwa kushirikiana na uongozi wa shule pamoja na Bodi ya shule kufanya maboresho ya vyoo vya wanafunzi pamoja na ukarabati wa nyumba za Walimu

Katika upande Mwingine alimpongeza Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Zungu kwa utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi pamoja na Mh,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, ambapo amewekeza sekta kwa kuboresha miundombinu ya shule na sekta ya afya.