November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule ya Sekondari zanaki wajivunia mafanikio

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Shule ya sekondari Zanaki iliyopo wilayani Ilala inajivunia mafanikio katika sekta ya maonesho ya kitaaluma imeweza kufanya vizuri kutokana na wanafunzi wa shule hiyo kuwa wabunifu.

Akizungumza wakati wa Mahafali ya wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Zanaki Mkuu wa shule hiyo Dellvine Koka,alisema wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wabunifu katika nyanja ya maonesho ya kitaaluma kimasomo kila idara wamefanya vizuri mwaka 2023.

“Wanafunzi wangu wamekuwa wabunifu wameandaa maonesho kwa dhumuni la kuwafanya wanafunzi waweze kuhamasisha maarifa waliokuwa nayo kutoka nadharia (Theory) hadi vitendo ambapo itawawezesha wanafunzi kuelewa umuhimu wa masomo yao kuelewa kwa upana na kutambua faida zinazopatikana katika masomo hayo hasa katika msingi wa elimu ya kujitegemea”alisema Koka.

Aidha alisema katika maonesho hayo wamekuwa wabunifu kila Idara ambapo wanafunzi wa Cookery wameweza kutengeneza keki na kuziuza na wanafunzi wa somo la ushonaji (Textile) wamebuni kutengeneza nguo,wanafunzi wa somo la uchoraji wameweza kutengeza thamani katika vikoi na kutengeneza logo.

“Wanafunzi wangu wa somo la Biashara wamebuni kutengeza ATM mashine za kutolea fedha pamoja na kuanzishwa Zahanati ya Student BANK kwa ajili ya kutoa huduma za kifedha idara ya sayansi somo la Kemia wametia fora wametengeza kiwi ya dawa ya viatu na kuziuza kwa wanafunzi wenzao na Wazazi .

Akizungumza katika Mahafali ya kidato cha nne ya shule hiyo alisema jumla ya wanafunzi 172 wanatarajia kuhitimu elimu ya sekondari ambapo alisema shule hiyo inafanya vizuri kila mwaka kitaaluma.

Alisema shule hiyo ya Zanaki imeweka mkakati wa kuondoa -ZIRO ambapo wanafunzi walionyesha bidii katika mitihani yao ya kujipima Mock ,NECTA Ilala na TAHOSA ni dhahiri wataenda kufanya vizuri mitihani ya Taifa aliwataka kuzingatia yale waliyofundishwa darasani na walimu wao .