Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Shule ya Sekondari Sangara iliyopo Mvuti kata Msongola wilayani Ilala , inajivunia mafanikio kitaaluma kwa miaka sita mfurulizo shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika ufaulu.
Akizungumza katika mahafali ya kumi na nne ya kidato cha nne shule ya sekondari Sangara wilayani Ilala Mkuu wa shule hiyo Frida Jacqline Nyoni, alisema maendeleo ya shule hiyo wamefanikiwa kitaaluma kutokana na ushirikiano Wazazi, Walimu na wanafunzi na kufanya vizuri kwa miaka sita mfurulizo.
“Shule yetu ya Sekondari Sangara tumefanya vizuri taaluma na kuongezeka ufaulu kwa miaka sita kuanzia mwaka 2017 kutokana na jitihada za kuinua ufaulu shuleni kwa ushirikiano wa Wazazi, wanafunzi na walimu wa shule yetu “Nyoni
Mkuu Frida Jaqline Nyoni, alisema kwa sasa mazingira ya shule hiyo mazuri kutokana na jitihada za Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan ,tuliweza kupokea msaada kutoka pochi la mama na kujengewa vyumba 14 vya madarasa .
Akizungumzia mahafali ya kumi na nne ya shule hiyo alisema jumla ya wahitimu 145 wanakabidhiwa vyeti kati yao wavulana 46 wasichana 99 wanafunzi hao wameandaliwa vizuri hivyo wanategemea kupata matunda mazuri mara watakapofanya mitihani yao ya Taifa ambapo inawapa matumaini kutokana na mitihani mbali mbali ambayo wamekuwa wakifanya ya majaribio
Akizungumzia mafanikio mengine alisema wamefanikiwa kupata pongezi kutoka Mfuko wa Elimu kwa ufaulu bora kwa mwaka 2017 mpaka sasa shule hiyo imekuwa ikifaulisha vizuri .
Akielezea msaada ambayo wamepata mingine alisema msaada wa kisima kirefu kutoka CDTF hiyo kwa ajili kujiandaa za kuinua ufaulu shuleni.
Kwa upande wa Mwakilishi,Mkuu wa Gereza Ukonga ASP Samwel Kuchela, aliwapongeza wahitimu wa shule hiyo kwa kuhitimu kidato cha nne na kuwataka wajiendeleze wakati wakisubiri matokeo yao kwani elimu aina mwisho.
Mwakilishi wa Gereza la Ukonga ASP Samwel Kuchela alitoa ahadi ya kusaidia Photocopy mashine kwa ajili ya shule hiyo
Aliwaasa wahitimu wa shule hiyo akiwambia ndoto za maisha na ufunguo wa maisha wanao wenyewe washirikiane na Wazazi katika maadili mema wasiingie katika mmomonyoko wa maadili ili ndoto zao ziweze kutimia waweze kuisaidia Serikali.
More Stories
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi