January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule ya Sekondari Mchanganyiko yajivunia mafanikio kitaaluma

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Shule ya Sekondari Mchanganyiko inajivunia mafanikio kitaaluma katika matokeo ya kidato cha nne kwa miaka mitatu mfululizo.

Akizungumza katika mahafali ya kumi na nne ya kidato cha nne Mkuu wa shule hiyo, Abeid Kamugisha, alisema mwaka 2022 matokeo ya kidato cha nne yaliotangazwa na NECTA shule ya Sekondari Mchanganyiko ilifanikiwa kufaulisha kwa asilimia 87 ambapo ni ongezeko la asilimia kumi ukilinganisha na ufaulu wa mwaka juzi .

“Shule yetu ya Sekondari Mchanganyiko inafanya vizuri kitaaluma katika mtihani wa Mock tuliweza kufaulisha kwa asilimia 86 .5 na mwaka huu tutafanya vizuri zaidi tuna matarajio makubwa kwani wanafunzi wameandaliwa vyema kufanya mitihani yao” alisema Kamugisha.

Mkuu Kamugisha alisema shule hiyo wana wanafunzi wa kidato cha nne wanaohitimu leo 450 kati yao wavulana 241 na wasichana 209,kidato cha pili ambao wanatarajia kufanya mitihani yao ya Taifa Octoba 30 mwaka huu Takwimu za NECTA mwaka jana 2023 ufaulu ulikuwa asilimia 91 hivyo ni matumaini yao wanafunzi wote watafanya vizuri katika mitihani yao.

Mkuu Kamugisha alisema shule hiyo inatokana na shule ya Msingi UHURU Mchanganyiko ambapo majengo ya shule ya msingi yaligawanywa na kuzalisha shule ya sekondari Mchanganyiko ambapo shule hiyo ilianza kuchukua wanafunzi Mei 2007 ikiwa na walimu nane wanafunzi 160 .

Aidha alisema kwa sasa shule ina Watumishi 37 wanaume 13 wanawake 24 na walimu wa kujitolea sita kwa upande wa wanafunzi 1588 kati yao wavulana ni 849 na wasichana 739.

“Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea madarasa matano ya UVIKO 19 na kuwapatia vifaa vya michezo ,vitabu vya kiada ,pesa za elimu bila malipo kila mwezi na mahitaji mengine muhimu ya uendeshaji wa shule “alisema

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Mtiti Mbasa aliwapongeza wanafunzi wa shule ya sekondari Mchanganyiko kwa kufanya vizuri kitaaluma ambapo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wanafunzi wa shule hiyo, walimu na wazazi kwa kufanya vizuri katika mitihani

Katibu Mtiti Mbasa aliwataka wahitimu wa shule hiyo wawe mabalozi wazuri huko wanapoenda wakatangaze shule hiyo yale mazuri ya sekondari ya Mchanganyiko kwani ni shule inayofanya vizuri kitaaluma.

“Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wa Wazazi Wilaya ya ilala leo Tarehe 19/10/2023 nimehudhuria Maafali ya 14 ya Kidato cha 4 Shule ya Secondary Mchanganyiko na kuwataka Wanafunzi wanaomaliza Shuleni hapo kuendelea na kiu ya kutaka kusoma zaidi,nawaomba Wazazi wa Watoto hawa
kuendelea kuwatunza Watoto wanu kwenye Mapenzi yenye Upendo kama Wazazi.”alisema Mtiti

Katibu Mtiti Mbasa amewataka Walimu na Wafanyakazi wa Shule hjyo kuendelea kuimarisha Upendo na mshikamano wao kwa Watoto ili kuenzi yale yote mazuri yanayofanywa na Walimu kama sehemu ya Wazazi wa Watoto hao.

*Katibu alisema Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya ilala itaendelea kuwa karibu na Shule hiyo kama Sehemu ya Majukumu yake kikanuni .

Alisema kwa niaba ya Serikali na Wazazi tunawaombea wote mfaulu mitihani yenu vizuri na ikiwezekana wote muendelee na masomo hadi vyuo vikuu

Aliwataka wazingatie sheria na miongozo ya shule pia wawe na heshima kwa walimu wao ,Wazazi, walezi ,na jumuiya nzima ya shule .